Ticker

6/recent/ticker-posts

TMA: Tahadhari juu ya Upepo mkali kutokea Leo,uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa



TMA: Tahadhari juu ya Upepo mkali kutokea Leo,uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi mashariki mwa Pwani ya Mtwara ambapo mifumo ya hali ya hewa iliyopo kwa sasa inaonesha kuwa mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kuimarika na kufikia hadhi ya kimbunga kamili Leo May 2, 2024.

TMA imesema wakati mgandamizo huo mdogo wa hewa ukiendelea kuimarika, unatarajiwa pia kusogea kuelekea baadhi ya maeneo ya Pwani ya Tanzania kuanzia usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa May 3, 2024 na kuendelea kuwepo katika maeneo ya ukanda huo hadi May 6,2024 kisha utapungua nguvu baada ya May 6, 2024.

“Uwepo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kutawala na kuathiri mifumo ya hali ya hewa hapa Nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro, Dar es salaam na maeneo ya jirani hivyo Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya Wataalamu katika Sekta husika ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza.

“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa chini na itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara kila inapobidi” – imeeleza taarifa ya TMA



Post a Comment

0 Comments