Utafiti: changamoto ya afya ya akili kwa vijana inaongezeka kwa kasi kubwa

Utafiti: changamoto ya afya ya akili kwa vijana inaongezeka kwa kasi kubwa

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shrika la Afya la Africa Academy for Public Health, Dk. Marry Sando, akizungumza wakati wa Warsha ya utafiti wa afya ya Akili kwa vijana, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Paul Sarea.

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk. Paul Sarea, amesema afya ya akili bado ni changamoto nchini hasa kwa rika la vijana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, amesema kuwa hali ya unyanyapaaji, hali ngumu ya maisha, mazingira kwa upande wa malezi na uelewa mdogo katika maisha, yamekuwa ni chachu kubwa inayosababisha wimbi hili la vijana kuanzia umri wa miaka 10-24 kupata afya ya akili.

Amesema kulingana na ripoti ya Shirika lisilo la serikali nchini Tanzania (AAPH), limebaini kuwa changamoto ya afya ya akili kwa vijana inaongezeka kwa kasi kubwa, ambapo hiyo inatokana na watu kutokuwa tayari kuzungumza matatizo yao na kuyahifadhi moyoni.

“Nakumbuka Sensa ya mwaka 2022 ilionyesha kuwa asilimia 19 ya idadi ya Tanzania ni vijana, wenye umri kati ya miaka 15-24, ambapo kundi hili tunalitegemea katika kutengeneza nguvu kubwa ya taifa, lakini bado kundi hili linaonekana kupata changamoto ya afya ya akili.

Pia, ametaja suala la mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kuwa yamekuwa chachu ya kusababisha watu kupata afya ya akili, ambapo hali hiyo inaweza kutokea na kusababisha mtu kupata mawazo pale anapokosa mahitaji yake maalumu.

Amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitengwa na kunyanyapaliwa kutokana na ugonjwa walioupata hivyo, husababisha kumuweka mtu huyo katika hali ya mawazo na wasiwasi na kupata tatizo la afya ya akili.

Kwa upende wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la (AAPH), Dk. Mary Sando, amesema Shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2009, limekuwa likifanaya kazi na serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, kwa kuangaliaa lishe ya afya ya mama na mtoto, kundi la vijana na matatizo ya afya ya akili.

Amesema mara kadhaa wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali kupitia mradi wao wa Being Tanzania na Ghana, ambao umekuwa ukiangalia ni kwa namna gani wataisaidia jamii kuepukana kutopata matatizo mbalimbali ya afya ya akili.

Naye  Mtafiti Mwandamizi wa (AAPH), Dk. Innocent Yusufu, ametoa rai kwa  vijana kuachana na  masuala ambayo ni hatarishi kwa upande wao yatayowapelekea kupata afya ya akili.

“Nitoe rai kwa vijana wenzangu kudumisha utamaduni wetu na tusikubali kutawaliwa na msongo wa mawazo, wasiwasi kwani hii ndiyo nguzo kubwa ya kusababisha suala la afya ya akili,” amesema Yusuph.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!