WHO:Niger kukabiliwa na ongezeko kubwa la homa ya uti wa mgongo au meningitis

WHO:Niger kukabiliwa na ongezeko kubwa la homa ya uti wa mgongo au meningitis

Niger ambayo mwaka huu inakabiliwa na ongezeko la asilimia 50 la wagonjwa wa homa ya uti wa mgongo au meningitis ikilinganishwa na mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO.

#SOMA Zaidi hapa kuhusu Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo au meningitis

Katika taarifa yake iliyotolea leo mjini Namey WHO inasema katika wiki ya 16 ya mwaka huu jumla ya wagonjwa 2012 wameripotiwa na vifo 123 ambalo ni ongezeko la asilimia 6.1 ya vifo ukilinganisha na wakati kama huo mwaka jana ambapo kulikuwa na wagonjwa 1,389 na vifo 72 na ongezeko hili la wagonjwa na vifo linatia wasiwasi mkubwa limesema shirika hilo la afya.

Kwa mujibu wa WHO eneo la Niamey ndilo kitovu cha janga hili, likiwa na kiwango cha jumla cha visa 52.2 kwa kila wakazi 100,000, ikifuatiwa na mikoa ya Agadez visa 11.5 kwa kila wakazi 100,000, Zinder wagonjwa 6.4 kwa kila kesi 100,000 na wakazi 6 kwa kila wenyeji 100,000.

Kanda ya afya Niamey I inasalia katika hali ya janga kwa wiki ya sita mfululizo, ikiwa na kiwango cha wastani wa wagonjwa 12.8 kwa kila wakazi 100,000. Wilaya zingine nane za afya pia zimevuka kizingiti cha tahadhari chawagonjwa 3 kwa kila wakaazi 100,000 katika wiki ya 16.

WHO na wadau wengine Kusaidia katika Janga Hili:

Wakati huu ambapo Niger inakabiliwa na hali hii mbaya, Shirika la Afya Duniani WHO, kwa ushirikiano na washirika mengine ya kiufundi na kifedha, wanafanya kazi kwa bidii kukabiliana na janga hili.

Hatua kadhaa zinaendelea, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa wagonjwa na uhamasishaji wa rasilimali kuandaa kampeni ya chanjo.

Kwa mujibu wa WHO chanjo dhidi ya homa ya uti wa mgongo imezinduliwa leo jana 2 Mei 2024 huko Niamey, kama sehemu ya juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Chanjo hii mpya ina faida ya kulinda dhidi ya aina tano za vichochezi vya homa ya uti wa mgongo ambavyo ni (A, C, W, X na Y), ambavyo ndio sababu kuu za homa ya uti wa mgongo nchini Niger.

Tofauti na chanjo za awali, WHO inasema chanjo hii mpya ni ya dozi moja.

Kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya uti wa mgongo inafanyika ili kuwa na Udhibiti wa mlipuko,

WHO inatoa msaada mkubwa kwenye usimamizi wa kesi kwa kuhakikisha dawa na nyenzo zingine muhimu zinapatikana.

Pia inaunga mkono uhamasishaji wa chanjo na kubeba gharama za uendeshaji kupitia ombi lililowasilishwa kwa Kikundi cha Kimataifa cha Kuratibu Chanjo (ICG).

Hatimaye, WHO inaratibu juhudi za washirika kusaidia nchi katika mapambano dhidi ya janga hili.

Kama utangulizi wa kampeni ya chanjo, WHO imeunga mkono idara ya ufuatiliaji na matokeo ya mlipuko katika kuandaa mafunzo ya vitendo kwenye uangalizi wa dawa kwa wasimamizi wa kitaifa wa kampeni na wasimamizi wa uangalizi wa dawa.

 WHO inatoa wito kwa washirika wote kuchukua hatua za haraka na zilizoratibiwa kushughulikia hali hii mbaya na kulinda idadi kubwa ya watu dhidi ya athari mbaya za homa ya uti wa mgongo.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!