Endometriosis Ni nini? Soma hapa Kufahamu

Endometriosis Ni nini? Soma hapa Kufahamu

Endometriosis ni tatizo linalohusisha Tishu kwenye ukuta wa kizazi(Uterus) kukua zaidi kuelekea nje. Ni ugonjwa ambao tishu zinazofanana na utando wa uterasi kukua nje ya uterasi,

Hali hii huweza kusababisha maumivu makali eneo la nyonga kwa mwanamke na kufanya iwe vigumu kwake kubeba ujauzito. Endometrosis ni tatizo Sugu linalohusishwa na;

  • maumivu makali wakati wa hedhi,
  • Maumivu wakati wa kujamiiana,
  • Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa na/au wakati wa kukojoa,
  • maumivu ya muda mrefu ya nyonga,
  • kuvimbiwa kwa tumbo
  • Kupata kichefuchefu,
  • uchovu,
  • na wakati mwingine mfadhaiko, wasiwasi,
  • Pamoja na tatizo la kutokubeba mimba/ugumba(Infertility).

Kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la afya Duniani(WHO); Tatizo la Endometriosis huathiri takriban asilimia 10% ya wanawake na wasichana duniani kote sawa na wanawake pamoja na Wasichana million 190 ambao wapo kwenye umri wa kuzaa Duniani kote.

Kwa sasa hakuna tiba ya moja kwa moja inayojulikana kwa ajili ya kutibu tatizo la endometriosis, Matibabu kwa kawaida hulenga kudhibiti dalili zake.

Kugunduliwa mapema na kuanza matibabu haraka ya endometriosis huleta matokeo chanya na ni muhimu sana kwa mwanamke mwenye tatizo hili,

Tatizo la Endometriosis ni Sugu,huweza kuanza toka unaanza Kupata hedhi yako ya kwanza mpaka unapofikia kipindi cha Ukomo wa hedhi(menopause).

Endometriosis ni ugonjwa wa uzazi unaohusishwa na hedhi ambapo tishu zinazofanana na ukuta wa tumbo la uzazi hupatikana katika maeneo mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na mirija ya uzazi, mfupa wa nyonga, uke na utumbo. Katika hali nadra, imepatikana hata kwenye mapafu, macho, mgongo na ubongo. Wakati mmoja ilifikiriwa kuwa mahali pekee katika mwili ambapo endometriosis haikutokea ni wengu, lakini mnamo 2020 ilipatikana huko pia .

Dalili ni pamoja na maumivu makali hadi ya kudhoofisha mwili mara nyingi katika eneo la mfupa wa nyonga/pelvic , uchovu, na hedhi nzito. Ingawa kuna hali nyingi za kiafya ambazo hazijulikani sana ambazo zina ufadhii mdogo wa kuzifahamu na hazijafanyiwa utafiti, chache ni za kawaida kama endometriosis, ambayo huathiri takriban watu 176m ulimwenguni .

Inakadiriwa kuwa 10% ya wanawake wana hali hii, ambayo inaweza kujumuisha maumivu makali ya kudhoofisha mwili. Lakini haijafanyiwa utafiti wa kutosha, haieleweki vizuri – na bado haina tiba.

Chanzo cha Tatizo la endometriosis

Sababu au chanzo cha tatizo la endometriosis hakijulikani. Pia Hakuna njia inayojulikana ya kuzuia endometriosis, na Hakuna tiba ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu tatizo hili, lakini dalili zake zinaweza kutibiwa kwa dawa au, katika hali nyingine, Upasuaji.

Endometriosis ni ugonjwa changamano (complex disease) ambao huwaathiri wanawake wengi duniani tangu mwanzo wa hedhi yao ya kwanza (menarche) hadi kukoma hedhi(menopause), bila kujali asili ya kikabila au hali ya kijamii.

Sababu nyingi tofauti hufikiriwa kuchangia tatizo hili au kuongeza hatari ya tatizo hili kutokea, Sababu hizo ni pamoja na;

1. Mwanamke kuwa na tatizo la Retrograde menstruation

Retrograde menstruation ni tatizo ambalo Damu ya hedhi kwa mwanamke yenye seli za Ukuta wa kizazi(endometrial cells) hutiririka na kurudi kwenye eneo la Pelvic Cavity kupitia kwenye mirija ya Uzazi(fallopian tubes) badala ya kutoka nje wakati wa hedhi,

Tatizo hili la Retrograde menstruation huweza kusababisha seli kutoka kwenye kuta za kizazi(endometrial-like cells) kujikusanya eneo la nje ya kizazi, ambapo huweza kujishikiza na kuendelea kukua Zaidi.

2. Tatizo la Cellular metaplasia ambapo seli za eneo la kizazi hubadilika kutoka kwenye muundo wa awali kwenda kwenye muundo mwingine,

Mwanamke mwenye shida hii,seli nje ya kizazi hubadilika na kuwa “endometrial-like cells” kisha kuanza kukua.

3. Kiwango cha baadhi ya Vichocheo mwilini(Mabadiliko ya hormones)

Tatizo la endometriosis huweza kutokea wakati kukiwa na mabadiliko ya vichocheo mwilini hasa vichocheo aina ya estrogen,

Ambapo hali hii huweza kuongeza Ukuaji wa seli,kuvimba n.k

Dalili za Tatizo la endometriosis

✓ Mara nyingi tatizo la Endometriosis husababisha maumivu makali ya kiuno/nyonga hasa wakati wa hedhi

✓ Baadhi ya wanawake wenye tatizo la endometriosis pia hupata maumivu wakati wa kujamiiana

✓ Au wakati wa kujisaidia haja kubwa na ndogo

✓ Baadhi ya wanawake wenye tatizo la endometriosis hupata shida ya kutokubeba Mimba(Infertility)

✓ Wanawake wengine wenye tatizo la endometriosis hawana dalili zozote. Kwa wale wenye dalili, Moja ya dalili ambazo hujitokeza sana ni pamoja na kupata maumivu katika sehemu ya chini ya tumbo (pelvis). Maumivu yanaweza kuonekana zaidi:

  • katika kipindi fulani wakati au baada ya tendo la ndoa
  • wakati wa kukojoa au kujisaidia haja kubwa n.k.

✓ Wanawake wengine pia hupata maumivu ya muda mrefu ya kiuno au nyonga(chronic pelvic pain)

✓ kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au katikati ya hedhi

✓ shida ya kupata mimba

✓ Tumbo kuvimbiwa na kujaa gesi(bloating)

✓ au kichefuchefu

✓ Kupata uchovu sana wa mwili

✓ Kuwa na mfadhaiko au wasiwasi.n.k

Dalili hizi mara nyingi hupungua au kuondoka baada ya Mwanamke kufikia Ukomo wa hedhi(menopause), lakini si mara zote.

Dalili za endometriosis huweza kuwa tofauti kati ya mtu na mtu,Pia zinaweza kufanana kabsa na dalili za magonjwa mengine hali ambayo husababisha kuwa vigumu kwa wafanyakazi wa afya kuzigundua kwa urahisi. Wanawake walio na dalili za tatizo la endometrosis wanaweza wasijue kuwa wana hali hiyo.

Matibabu ya Tatizo la endometriosis

Matibabu ya kudhibiti endometriosis yanaweza kutofautiana kulingana na ukali wa dalili na ikiwa Mwanamke mwenye tatizo hili anahitaji kubeba mimba.

Fahamu kwamba,Hakuna matibabu ya kutibu kabsa ugonjwa huu, ila kuna matibabu ya kudhibiti dalili zake.

✓ Baadhi ya dawa  huweza kutumika kwa mwanamke mwenye tatizo hili La endometriosis ikiwemo;

  • Dawa za maumivu jamii ya Non-steroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) and analgesics (painkillers)  kama vile ibuprofen pamoja na naproxen
  • Dawa za hormones kama vile Contraceptive Pills n.k
  • Dawa za kukusaidia kubeba Ujauzito,kwa wale wanaohitaji mtoto n.k

✓Kufanyiwa UPASUAJI. n.k

Kumbuka; Kama una dalili za tatizo hili hakikisha unafanya vipimo na Kuanza Tiba Mapema au;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!