Mahujaji 14 wa Hajj kufariki dunia kisa joto kali
Takriban raia 14 wa Jordan wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia kutokana na joto kali, maafisa wamesema.
Wizara ya mambo ya nje ya Jordan ilisema raia wake 14 wamefariki “baada ya kupigwa na jua sana kutokana na wimbi la joto kali” na wengine 17 wameripotiwa kupotea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Shirika la Red Crescent la Iran limethibitisha kuwa mahujaji watano wa Iran pia wamepoteza maisha, lakini haikueleza jinsi walivyofariki.
Maafisa wa Jordan walisema msako unaendelea kuwatafuta waliotoweka.
Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje ya Jordan ilisema kuwa inawasiliana na mamlaka ya Saudia kuhusu taratibu za kuzika au kusafirisha miili ya marehemu, kulingana na matakwa ya familia zao.
Hajj ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya watu duniani ambapo zaidi ya mahujaji milioni 1.8 wanashiriki hijja mwaka huu, kulingana na maafisa wa Saudi.
Lakini ina historia ya majanga makubwa ikiwa ni pamoja na mikanyagano na moto wa mahema. Lakini kwa miaka mingi, changamoto kuu hutokana na joto kali.
Halijoto wiki hii ilizidi 46C (114.8F) na kufanya tamaduni nyingi zinazofanywa nje na kwa miguu kuwa na changamoto hasa kwa wazee
Via:Bbc
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!