WHO: Zaidi ya wanawake 600,000 kuishi na matokeo mabaya ya UKEKETAJI
Inakadiriwa kuwa wasichana milioni 4.3 walikuwa hatarini kukabiliwa na ukeketaji mwaka 2023.
Utafiti huo uliohusisha taarifa zilisowasilishwa na nchi pamoja na asasi za kiraia umebainisha kuwa ingawa mataifa mengi yameongeza juhudi za kutokomeza ukeketaji lakini tabia hiyo inaendelea duniani kote kwa siri kwa kuwavusha mipaka wasichana kwenda kueafanyia ukeketaji kimataifa.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk akizungumzia ripoti hiyo amesema “ Ukeketaji ni sehemu ya mwendelezo wa ukatili wa kijinsia na hauna nafasi katika ulimwengu unaoheshimu haki za binadamu.
Ripoti hiyo imezitaka nchi kuhakikisha wanaweka njia za kuzuia vitendo hivyo na kutengeneza mazingira ya kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukeketaji kwa kushirikiana na asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali, jamii, bila kusahau viongozi wa dini na viongozi wengine ndani ya jamii.
Shirika la afya ulimwenguni (WHO) linataja zaidi ya wanawake 600,000 kutoka Muungano wa Ulaya wanadhaniwa kuishi na matokeo ya ukeketaji huku shirika hilo likieleza kuwa taratibu zote zinazohusisha kuondoa sehemu au viungo vya jinsia ya kike, au kusababisha madhara mengine kwenye viungo vya jinsia ya kike kwa sababu zisizo za kitiba ni uvunjifu wa haki za binadamu.
“kitendo hiki hakina faida kiafya kwa wasichana na wanawake na husababisha kutokwa damu kwa wingi, matatizo ya mkojo na maambukizi, pamoja na matatizo wakati wa kujifungua na hatari zaidi ya vifo vya watoto wachanga,” WHO.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!