Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
Baada ya kufanyiwa Upasuaji wa kujifungua kwa kitaalam Cesarean Section(C-Section), Moja ya vitu muhimu vya kuzingatia ni hali ya kidonda chako,
Unashauriwa kukitunza kidonda kwa uangalifu ili kisipate Maambukizi yoyote(infections), na Ukiona Dalili hizi hakikisha unapata Msaada mapema;
1. Kuvimba eneo la kidonda ulipofanyiwa upasuaji
2. Kidonda kuanza kuvuja maji maji
3. Kidonda kuvuja Damu
4. Kupata maumivu makali sana ya kidonda ambayo hayaishi hata baada ya kutumia dawa
5. Sehemu ya Kidonda kubadilika rangi na kuwa nyekundu Sana(Redness around the incision)
6. Kidonda kutoa harufu mbaya n.k
Vitu ambavyo huongeza hatari ya kupata madhara wakati wa kujifungua kwa Upasuaji
Ingawa ni mara chache sana kutokea,ila vitu hivi huweza kuchangia madhara;
– Mtoto kuwa Mkubwa Sana
– Mama kuwa Mnene kupita kiasi
– Kuwa na Labor ya Muda mrefu Zaidi
– Kuwa na Mzio au Allergies na dawa za USINGIZI
– Damu yako kuwa ndogo Sana
– Kuwa na magonjwa kama vile Kisukari n.k
#SOMA hapa kwanini Wanawake wengi hujifungua kwa Upasuaji?
Madhara ya Kujifungua kwa Upasuaji(Complications)
Haya ni baadhi ya madhara ambayo huweza kutokea baada ya kujifungua kwa Upasuaji;
• Maambukizi ya kidonda
• Kupata homa
• Kupoteza damu nyingi
• Kupata majeraha kwa baadhi ya viungo(organs)
• Hali ya Dhararua inayopelekea utolewe kabsa kizazi(emergency hysterectomy)
• Kupata madhara kutokana na kuwa na allergy au mzio na dawa za Usingizi
• Mtoto kudhurika wakati wa Upasuaji
• Mama kupoteza Maisha N.k
Kwa bahati nzuri, matatizo makubwa kutokana na kujifungua kwa upasuaji ni nadra sana kutokea. Katika nchi zilizoendelea, vifo vinavyotokana na uzazi ni nadra sana kutokea.
Na Mara nyingi vifo havihusiani na kitendo cha Upasuaji bali vinahusiana na matatizo ya ujauzito ambayo hukufanya kuzaa kwa upasuaji.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!