kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
Unapopata tatizo la kuharisha na kutapika kwa wakati mmoja unaweza kuwaza sana, shida ni nini mbona vyote hivi hutokea kwa Wakati mmoja.
Mara nyingi Kutapika na kuharisha kwa wakati mmoja hutokea kwa ugonjwa unaosababishwa na virusi au maambukizi ya bakteria ambayo huathiri mfumo wako wa usagaji chakula. Lakini dalili hizi zinaweza kutokea Kwa hali zingine za kiafya pia.
Chanzo cha kuharisha na kutapika kwa wakati mmoja
Zipo Sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii ikiwemo;
Maambukizi ya Vimelea kama Virusi au bacteria kwenye Mfumo mzima wa chakula(gastrointestinal (GI) infection)
Hii ni miongoni mwa Sababu kubwa ya Mtu kupata dalili ya kuharisha na kutapika kwa wakati mmoja.
1. Maambukizi ya Virusi
Mfano wa maambukizi ya Virusi kwenye Utumbo(Viral gastroenteritis) ambayo huweza kusababisha tatizo la kutapika na kuharisha kwa wakati mmoja ni pamoja na virusi kama;
- norovirus
- rotavirus
- adenovirus
- astrovirus
Virusi hivi hupitishwa kutoka kwa mtu hadi mtu kwa kugusa kinyesi kilichoambukizwa na matapishi. Hii inaweza kutokea wakati mtu aliye na maambukizi haya hanawi mikono yake vizuri baada ya kutumia choo na kisha kugusa sehemu zinazotumiwa na watu wengine au kuandaa chakula kwa ajili ya wengine.
2. Chakula kuchafuliwa au kuwa na Sumu,Food poisoning
Hapa tunazungumzia zaidi maambukizi ya bacteria kwenye mfumo mzima wa chakula baada ya mtu kula chakula chenye vimelea hawa,
Kwa Asilimia kubwa Food poisoning huhusisha bacteria ingawa pia vimelea kama parasites au virusi huweza kuwa chanzo.
Unaweza kupata sumu kwenye chakula kwa kula chakula kilichochafuliwa. Hili linaweza kutokea nyumbani au kwenye migahawa wakati chakula kinapoandaliwa kwenye mazingira machafu, vibaya au hakijapikwa ipasavyo.
Hawa ni aina ya bacteria ambao huhusika na Food poisoning kwa kiasi kikubwa;
- E. coli
- Campylobacter
- Listeria monocytogenes
- Salmonella
- Shigella
- Staphylococcus aureus
Dalili za sumu kwenye chakula zinaweza kuanza ndani ya saa chache baada ya kula chakula kilichochafuliwa na mara nyingi huisha baada ya saa chache hadi siku chache. Hii kawaida hufanyika bila matibabu maalum.
Kutapika na kuharisha maji ni dalili kubwa. Dalili zingine ni pamoja na:
– maumivu ya tumbo
– kichefuchefu
– homa
– kuhara damu n.k
3. Tatizo la kuharisha kwa wasafiri au Traveler’s diarrhea
Traveler’s diarrhea ni ugonjwa wa njia ya usagaji chakula ambao mara nyingi husababishwa na virusi, vimelea kama parasites, au bakteria ambao unawapata kwenye maji au chakula.
Kuna uwezekano mkubwa wa hali hii kutokea pale unapotembelea eneo lenye hali ya hewa tofauti au usafi wa mazingira kuliko yale uliyozoea nyumbani.
Traveler’s diarrhea; kwa ujumla huisha ndani ya wiki 1. Kuharisha maji maji na tumbo kuuma ni dalili za kawaida, lakini tatizo hili la kuharisha kwa wasafiri au Taveler’s diarrhea hunaweza pia kusababisha:
- kichefuchefu
- homa
- gesi tumboni
- uvimbe
- Hitaji la haraka la kwenda kujisaidia haja kubwa n.k
4. Msongo wa mawazo au Wasiwasi, Stress or anxiety
Tafiti zinaonyesha kuwa na wasiwasi sana, hofu kubwa au Stress huweza kupelekea mabadiliko mengi mwilini ikiwemo kukuletea hali kama hizi;
- Kuharisha na kutapika
- Kichefuchefu
- Kupata choo kigumu sana
- Kukosa choo kabsa
- Maumivu ya Tumbo
- Kupata kiungulua n.k
Hii ni kwasababu stress hormones au Vichocheo vinavyohusika na mfadhaiko au msongo wa mawazo vinatolewa na mwili wako polepole katika tumbo lako na utumbo mdogo. Pia husababisha kuongezeka kwa motility katika utumbo wako mkubwa.
Na hapa ndipo unaanza kuona mabadiliko na dalili nyingi kwenye mfumo mzima wa chakula.
5. Ujauzito
Kipindi cha Ujauzito mwili wako hupokea mabadiliko mengi sana kutokana na mabadiliko makubwa ya Vichocheo vya Mwili(hormonal changes),
Hivo kwa baadhi ya Wanawake huweza kupata dalili hii pia ya kuharisha na kutapika kipindi cha Ujauzito
6. Kula au kunywa Kupita kiasi,
Fahamu kwamba kula na kunywa kupita kiasi huweza kusababisha utapike na uharishe pia, Na mara nyingi unaweza kupata dalili zingine kama vile;
- Kiungulia
- Tumbo kujaa gesi
- Tumbo kuuma n.k
Uhusiano kati ya pombe na utumbo: Baadhi ya aina za pombe, ikiwa ni pamoja na vinywaji vyenye sukari, zinaweza kusababisha kuharisha kwa kushawishi njia ya utumbo kupitisha vitu haraka. Hii inapunguza usagaji wa chakula, kwani utumbo hauna wakati wa kunyonya virutubishi au vitu vingine ambavyo hupita kwa haraka.
Unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kusababisha ugonjwa unaojulikana kama alcoholic gastritis, ambapo huhusisha muwasho wa utando wa tumbo. Ugonjwa wa gastritis unaweza kutokea baada ya kunywa kupita kiasi, au ugonjwa wa gastritis unaweza kuwa sugu kwa watu wanaokunywa pombe mara kwa mara.
Gastritis ikitokea huweza kuambatana na dalili hizi:
- Maumivu ya Tumbo upande wa juu
- Au kuhisi hali ya kuungua tumboni
- Kiungulia
- Kujaa gesi tumboni n.k
7. Matumizi ya baadhi ya dawa,
Kutapika na kuharisha ni madhara ya dawa nyingi. Baadhi ya Dawa Zina uwezekano mkubwa Zaidi wa kusababisha dalili hizi kuliko Zingine.
Hii inaweza kuwa kwa sababu ya jinsi dawa inavyofanya kazi au kwa sababu zina viambatanisho vinavyokera tumbo.
Umri wako, afya kwa ujumla, na dawa zingine pia zinaweza kuongeza hatari ya athari.
Dawa ambazo mara nyingi husababisha kutapika na kuharisha ni pamoja na:
– Baadhi ya antibiotics
– Dawa jamii ya nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDS),kama vile ibuprofen (Advil, Motrin) na aspirini.
– dawa za chemotherapy
– metformin (Fortamet, Glumetza) n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!