Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara ya kuweka kope bandia,Fahamu hapa



Madhara ya kuweka kope bandia,Fahamu hapa

Kope zetu za asili hufanya kazi muhimu, hulinda macho yetu kwa kuelekeza hewa mbali na mboni ya jicho, na kutufanya kupepesa, hatua ambayo pia huhakikisha kwamba macho yana majimaji vizuri.

Kope bandia hushikanishwa na kila kope asili, moja kwa moja.

Kope hizi huunganishwa na gundi ambayo inaweza kusababisha matatizo.

Wataalamu wengi wa vipodozi hufanya jaribio la awali la kiraka cha kope bandia kwenye eneo fulani la mwili, kwa kawaida kwenye mkono au nyuma ya sikio, ili kuangalia mizio ya gundi; hata hivyo, hata ikiwa hakuna athari ya mzio(Allergy), kemikali katika gundi inaweza kuwasha eneo la jicho na uzito wa gundi yenyewe inaweza kusababisha muwasho kwenye kope.

Matumizi sahihi ni muhimu. Kumekuwa na ripoti za watu ambao kope zao zimeshikamana kwasababu ya matumizi ya kope bandia.

Kwa mujibu wa utafiti mmoja, zaidi ya asilimia 60 ya wanawake waliripoti changamoto ya keratoconjunctivitis, hali ya jicho inayohusisha kuvimba kwa kornea na kiwambo cha jicho kwa wakati mmoja, baada ya gundi ya kope bandia kugusa macho yao.

Utafiti huo huo uligundua kuwa asilimia 40% ya wanawake walipata athari ya mzio kwasababu ya gundi.

Gundi inayosababisha saratani

Kumekuwa na nyakati ambapo gundi ya kucha, ambayo ina nguvu zaidi imeuzwa kama gundi ya kope.

Katika mojawapo ya matukio ya kushtua sana ya utumiaji usiofaa, kope za mwanamke ziliachwa zikiwa zimeshikamana pamoja baada ya kuweka kope bandia kwa kutumia gundi kali.

Gundi ya kope inaweza kusababisha hatari kadhaa za afya. Utafiti mmoja ulichanganua viambata 37 vya kibiashara na kitaalamu na kugundua uwepo wa formaldehyde, kemikali inayojulikana kusababisha saratani.

Uchambuzi huo uligundua kuwa asilimia 75 ya viambata 20 vya kitaalamu vilivyojaribiwa vilitoa formaldehyde, na gundi nne kati ya 17 za kibiashara pia zilikuwa na kemikali hiyo.



Post a Comment

0 Comments