Mgonjwa wa Saba Apona Ugonjwa wa Ukimwi

Mgonjwa wa Saba Apona Ugonjwa wa Ukimwi

Mwanaume mmoja wa Ujerumani aliye na umri wa miaka 60, huenda akawa Mtu wa saba kupona Virusi vya Ukimwi baada ya kupandikizwa Uloto ambapo Mjerumani huyo ambaye ametaka kutotajwa jina, amepachikwa jina la “mgonjwa anayefuata wa Berlin”.

Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa Daktari Mtafiti katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Charite cha Berlin Christian Gaebler, amesema Timu yao haiwezi kuthibitisha kwa uhakika ikiwa virusi vya VVU vimetokomezwa kabisa kwa Mgonjwa huyo.

Mgonjwa wa awali wa Berlin, Timothy Ray Brown, alikuwa Mtu wa kwanza kutangazwa kuponywa VVU mnamo mwaka 2008, hata hivyo, Brown alifariki kutokana na saratani mwaka 2020.

Mwanaume huyo anayetajwa kuwa wa saba kupona VVU aligunduliwa mara ya kwanza kuwa na maambukizi ya VVU mwaka 2009.

Mafanikio ya upandikizaji Seli Shina kwa Watu wenye VVU, yametangazwa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa 25 wa kimataifa wa UKIMWI katika Mji wa Munich mapema wiki ijayo.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!