Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya, wengi miongoni mwao ni wanaume.
Ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha kwamba vifo milioni 2.6 kila mwaka vilitokana na unywaji pombe, ambayo ni asilimia 4.7 ya vifo vyote, na vifo milioni 0.6 kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.Vifo milioni 2 kwa watumiaji wa pombe na milioni 0.4 ya vifo vinavyotokana na madawa ya kulevya vilikuwa miongoni mwa wanaume.
Ripoti ya hali ya Ulimwenguni kutoka WHO kuhusu pombe na afya, Na matibabu ya matatizo ya matumizi ya dawa za kulevyia hutoa Taarifa pana kulingana na data za mwaka 2019 kuhusu athari za afya ya umma kwenye matumizi ya pombe na dawa za kulevya na hali ya unywaji pombe na matibabu ya matatizo ya matumizi ya dawa za kulevyia duniani kote.
Ripoti hiyo inaonyesha takriban watu milioni 400 waliishi na matatizo yanayotokana na matumizi ya pombe duniani. Kati yao,watu milioni 209 waliishi na utegemezi wa pombe.
“Matumizi ya dawa za kulevyia hudhuru sana afya ya mtu binafsi, huongeza hatari ya magonjwa sugu, hali ya afya ya akili, na kwa kusikitisha Zaidi husababisha mamilioni ya vifo vinavyoweza kuzuilika kila mwaka,
Huweka mzigo mzito kwa familia na jamii, na kuongeza uwezekano wa ajali, majeraha na vurugu, Alisema Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO. “Ili kujenga jamii yenye afya na usawa zaidi, ni lazima tujitolee kwa haraka kuchukua hatua za kijasiri ambazo zitapunguza matokeo mabaya ya kiafya na kijamii ya unywaji pombe na kufanya matibabu ya matatizo yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevyia kupatikana na yawe ambayo mtu anaweza kumudu.”
Ripoti hiyo inaangazia hitaji la dharura la kuharakisha Kwa hatua ulimwenguni kote kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) lengo la 3.5 ifikapo 2030 kwa kupunguza matumizi ya pombe na dawa za kulevya na kuboresha upatikanaji wa matibabu bora kwa matatizo ya matumizi ya dawa.
Matokeo ya kiafya ya unywaji pombe
Ripoti hiyo inaangazia kwamba licha ya kupungua kwa viwango vya vifo vinavyotokana na pombe tangu 2010, idadi ya jumla ya vifo kutokana na unywaji pombe bado ni juu,hali isiyokubalika na inafikia milioni 2.6 mnamo 2019, na idadi kubwa zaidi ni katika Kanda ya Ulaya na kanda ya Afrika.
Viwango vya vifo vinavyotokana na unywaji pombe kwa lita moja ya pombe inayotumiwa ni vya juu zaidi katika nchi zenye mapato ya chini,na chini kabisa katika nchi zenye mapato ya juu.
Kati ya vifo vyote vilivyotokana na pombe mwaka wa 2019, inakadiriwa vifo milioni 1.6 vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza, vikiwemo vifo 474,000 kutokana na magonjwa ya moyo na mishipa na 401,000 kutokana na saratani.
Baadhi ya vifo 724,000 vilitokana na majeraha, kama vile ajali za barabarani, kujidhuru na ghasia kati ya watu. Vifo vingine 284,000 vilihusishwa na magonjwa ya kuambukiza. Kwa mfano, unywaji wa pombe umeonyeshwa kuongeza hatari ya maambukizi ya VVU kutokana na kuongezeka kwa hatari ya kujamiiana bila kinga na kwa kuongeza hatari ya kuambukizwa TB na vifo vinavyotokana na Kinga ya Mwili kuwa dhaifu Sana.
Sehemu kubwa zaidi (13%) ya vifo vilivyotokana na pombe mnamo 2019 vilikuwa kati ya vijana wenye umri wa miaka 20-39.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!