AINA ZA UCHAFU UNAOTOKA UKENI,RANGI NA DALILI ZAKE

 AINA ZA UCHAFU UNAOTOKA UKENI,RANGI NA DALILI ZAKE

Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii huashiria kwamba kuna tatizo ukeni, na katika makala hii tumechambua aina mbali mbali za uchafu ukeni kwa kuangalia rangi zake na dalili za magonjwa.

1. UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU

Huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevurugika na wakati mwingine ni dalili ya magonjwa kama kansa ya kizazi,

mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi pamoja na kuumwa sana nyonga, hivo ukiona dalili kama hizi nenda kafanye vipimo hospital na kuanza tiba mapema

2. UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA

Endapo uchafu huo utatoka kama povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas,PID(pelvic inflammatory disease), maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe,

dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo,maumivu wakati wa tendo la ndoa,kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo la ndoa n.k.

3. UCHAFU MWEUPE MZITO KAMA JIBINI

Mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

Ngozi ya eneo la nje kubadilika rangi na kuwa nyekundu,kuhisi hali ya kuungua wakati wa kutembea,

uchafu mzito kutoka ukeni na wa rangi mithili ya maziwa mgando,uchafu huu huweza kuambatana na harufu mbaya kutoka ukeni

4. UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI

Uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nje ya uke.

KUMBUKA: Jua kutofautisha kati ya ute ute ambao ni kawaida kumtoka mwanamke akiwa kwenye siku za hatari na aina za uchafu unaotoka ukeni ambao nimetoa maelezo yake.

Ute ute wa siku za hatari unakuwa wa kuvutika kama vile ule wa kwenye yai la kuku,na hauna harufu yoyote mbaya

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!