Azithromycin inatibu magonjwa gani
Katika Makala hii tumechambua baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa kwa kutumia dawa ya Azithromycin.
Azithromycin ni dawa jamii ya antibiotic ambayo hutumika kutibu aina mbali mbali za maambukizi ya bacteria kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo;
- Kwenye masikio
- Kwenye ngozi
- Kwenye koo
- Kwenye Njia ya Mkojo n.k
Hivo basi, kwa ujumla Azithromycin hutibu maambukizi ya bacteria na sio maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Virus.
Azithromycin inatibu magonjwa gani
Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ambayo dawa ya Azithromycin huweza kutibu;
- Azithromycin huweza kutumika kwenye matibabu ya Ugonjwa wa UTI, hapa tunazungumzia maambukizi ya bacteria kwenye mfumo wa mkojo ikiwemo;
- Kwenye njia ya mkojo,
- kibofu cha mkojo,
- figo n.k
- Azithromycin huweza kutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya bacteria kwenye Mapafu(pneumonia)
- Azithromycin huweza kutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya Zinaa kama vile Kisonono(gonorrhoea) pamoja na chlamydia
Hivo basi,Azithromycin pia huweza kutumika kwenye matibabu ya magonjwa ya zinaa kama vile;
- matibabu ya ugonjwa wa Kisonono,
- Ugonjwa wa chlamydia
- Azithromycin huweza kutumika kwenye Matibabu ya ugonjwa wa homa ya matumbo au typhoid
- Azithromycin huweza kutumika kwenye matibabu ya tatizo la chancroid n.k
Maudhi madogo madogo(Side effects) kwenye Matumizi ya Dawa ya Azithromycin
Haya hapa ni baadhi matokeo ambayo huweza kujitokeza baada ya kutumia dawa ya Azithromycin kwa baadhi ya watu;
- Kupata maumivu ya kichwa
- Kuhisi kizunguzungu
- Kuhisi kichefuchefu
- Kupata maumivu ya tumbo
- Kuharisha n.k
Tahadhari(Warnings) kwenye Matumizi ya dawa ya Azithromycin
✓ Usitumie dawa ya Azithromycin kama unapata allergic reactions dhidi ya azithromycin au antibiotic zingine kwenye kundi moja kama vile erythromycin n.k
✓ Kama ni mjamzito au unanyonyesha,hakikisha kabla ya kutumia dawa ya Azithromycin unapewa maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya
✓ Dawa ya Azithromycin inaweza kuleta hali ya kizunguzungu,hivo unashauriwa kuepuka kufanya kazi za hatari ikiwemo kuendesha gari barabarani kama umetumia dawa hii ya Azithromycin na hujisikii vizuri.
✓ Epuka kutumia Pombe wakati wa matumizi ya dawa ya Azithromycin,
Kwani hii huweza kuzidisha maudhi(side effects) ya dawa ya Azithromycin ikiwemo;
- kizunguzungu
- Pamoja na kusinzia
✓ Ongea kwanza na wataalam wa afya kabla ya matumizi ya dawa ya Azithromycin kama una matatizo kama haya;
Matatizo ya Moyo
Matatizo ya Ini
Matatizo ya Figo
Matatizo ya afya ya akili
Hali yoyote ambayo hudhoofisha misuli ya mwili (myasthenia gravis).
Kama una tatizo la kuharisha sana na kwa muda mrefu baada ya kutumia dawa ya Azithromycin
Kama una tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha potassium au magnesium kwenye damu n.k.
Hitimisho
Azithromycin ni dawa jamii ya antibiotic ambayo hutumika kutibu aina mbali mbali za maambukizi ya bacteria kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo;
- Kwenye masikio
- Kwenye ngozi
- Kwenye koo
- Kwenye Njia ya Mkojo n.k
Dawa ya Azithromycin huweza kuleta maudhi(side effects) kwa baadhi ya watu ikiwemo;
Kupata maumivu ya kichwa,Kuhisi kizunguzungu,Kuhisi kichefuchefu, Kupata maumivu ya tumbo,Kuharisha n.k
Pia Epuka matumizi ya dawa ya Azithromycin kama unapata allergic reactions dhidi ya azithromycin au antibiotic zingine kwenye kundi moja kama vile erythromycin n.k
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!