Ticker

6/recent/ticker-posts

Azuma inatibu magonjwa gani,Soma hapa kufahamu



Azuma inatibu magonjwa gani,Soma hapa kufahamu

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa kwa kutumia dawa ya Azuma.

Azuma ni dawa jamii ya antibiotic ambayo hutumika kutibu aina mbali mbali za maambukizi ya bacteria kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo;

  • Kwenye masikio
  • Kwenye ngozi
  • Kwenye koo
  • Kwenye Njia ya Mkojo n.k

Hivo basi, kwa ujumla Azuma hutibu maambukizi ya bacteria na sio maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Virus.

Azuma inatibu magonjwa gani

Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ambayo dawa ya Azuma huweza kutibu;

- Azuma huweza kutumika kwenye matibabu ya Ugonjwa wa UTI, hapa tunazungumzia maambukizi ya bacteria kwenye mfumo wa mkojo ikiwemo;

  • Kwenye njia ya mkojo,
  • kibofu cha mkojo,
  • figo n.k

- Azuma huweza kutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya bacteria kwenye Mapafu(pneumonia)

- Azuma huweza kutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya Zinaa kama vile Kisonono(gonorrhoea) pamoja na chlamydia

Hivo basi,Azuma pia huweza kutumika kwenye matibabu ya magonjwa ya zinaa kama vile;

  • matibabu ya ugonjwa wa Kisonono,
  • Ugonjwa wa chlamydia

- Azuma huweza kutumika kwenye Matibabu ya ugonjwa wa homa ya matumbo au typhoid

- Azuma huweza kutumika kwenye matibabu ya tatizo la chancroid n.k

Maudhi madogo madogo(Side effects) kwenye Matumizi ya Dawa ya Azuma

Haya hapa ni baadhi matokeo ambayo huweza kujitokeza baada ya kutumia dawa ya Azuma kwa baadhi ya watu;

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kuhisi kizunguzungu

- Kuhisi kichefuchefu

- Kupata maumivu ya tumbo

- Kuharisha n.k

Tahadhari(Warnings) kwenye Matumizi ya dawa ya Azuma

✓ Usitumie dawa ya Azuma kama unapata allergic reactions dhidi ya azithromycin au antibiotic zingine kwenye kundi moja kama vile erythromycin n.k

✓ Kama ni mjamzito au unanyonyesha,hakikisha kabla ya kutumia dawa ya Azuma unapewa maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya

✓ Dawa ya Azuma inaweza kuleta hali ya kizunguzungu,hivo unashauriwa kuepuka kufanya kazi za hatari ikiwemo kuendesha gari barabarani kama umetumia dawa hii ya Azuma na hujisikii vizuri.

✓ Epuka kutumia Pombe wakati wa matumizi ya dawa ya Azuma,

Kwani hii huweza kuzidisha maudhi(side effects) ya dawa ya azuma ikiwemo;

  • kizunguzungu
  • Pamoja na kusinzia

✓ Ongea kwanza na wataalam wa afya kabla ya matumizi ya dawa ya Azuma kama una matatizo kama haya;

Matatizo ya Moyo

Matatizo ya Ini

Matatizo ya Figo

Matatizo ya afya ya akili

Hali yoyote ambayo hudhoofisha misuli ya mwili (myasthenia gravis).

Kama una tatizo la kuharisha sana na kwa muda mrefu baada ya kutumia dawa ya Azuma

Kama una tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha potassium au magnesium kwenye damu n.k.

Hitimisho

Azuma ni dawa jamii ya antibiotic ambayo hutumika kutibu aina mbali mbali za maambukizi ya bacteria kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo;

  • Kwenye masikio
  • Kwenye ngozi
  • Kwenye koo
  • Kwenye Njia ya Mkojo n.k

Dawa ya Azuma huweza kuleta maudhi(side effects) kwa baadhi ya watu ikiwemo;

Kupata maumivu ya kichwa,Kuhisi kizunguzungu,Kuhisi kichefuchefu, Kupata maumivu ya tumbo,Kuharisha n.k

Pia Epuka matumizi ya dawa ya Azuma kama unapata allergic reactions dhidi ya azithromycin au antibiotic zingine kwenye kundi moja kama vile erythromycin n.k





Post a Comment

0 Comments