Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANZO CHA KITOVU CHA MTOTO KUCHELEWA KUDONDOKA



 Kitovu cha mtoto yaani Umbilical cord hufanya kazi muhimu sana kwenye maisha ya mtoto kwani ndicho hupitisha virutubisho vyote yaani Nutrients kutoka kwa mama kwenda mtoto pamoja na hewa safi ya Oxygen wakati mtoto akiwa tumboni,Lakini baada ya mtoto kuzaliwa huanza kujitegemea mwenyewe kwa kila kitu,hivo mifumo kama hii haihitajiki tena kwa mtoto.

Baada ya mtoto kuzaliwa hukaa kwa muda flani ndipo kitovu hukauka na kudondoka chenyewe kama ilivyokawaida,japo kuna watoto wengine huwahi zaidi na kuna baadhi yao kitovu huchelewa sana kudondoka, Watoto wengi kitovu hudondoka chenyewe ndani ya kipindi cha Wiki 1 mpaka 2 baada ya kuzaliwa, japo kwa watoto ambao walizaliwa kabla ya wakati yaani PREMATURE BABY kitovu kudondoka huweza kuchukua muda mrefu kidogo kama vile kipindi cha wiki 2 mpaka 3.

Hivo mama wa mtoto hushauriwa kumchunguza mtoto wake katika kipindi hiki ili kuhakikisha kitovu cha mtoto hakiwi na maambukizi yoyote ya magonjwa.Vitu vya muhimu kuangaliwa kwa mtoto ni pamoja na kuhakikisha kitovu hakivuji damu muda mchache baada ya mtoto kuzaliwa,kitovu hakitoi usaha,harufu au kubadilika rangi,

CHANZO CHA KITOVU CHA MTOTO KUCHELEWA KUDONDOKA

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia kitovu cha mtoto kuchelewa kudondoka, na sababu hizo ni pamoja na;

- Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati yaani Premature birth

-Tatizo la Leukocyte Adhesion Deficiency type 1 (LAD-1)

- Matatizo mbali mbali pamoja na hitilafu katika utendaji kazi wa PMNL na Chemotaxis mfano; Shida ya urachal abnormalities, LAD-1 n.k

- Tatizo la Necrosis,ukaukaji wa Kitovu, Matatizo ya utendaji kazi wa Collagenase n.k

KUMBUKA: Kitovu cha mtoto kinatakiwa kutunzwa kwa umakini mkubwa,epuka kupaka vitu mbali mbali kwenye kitovu cha mtoto kwa lengo la kusaidia kikauke.

MAMBO YA KUZINGATIA KWA MTOTO WAKO

• Hakikisha mtoto ananyonya vizuri kwa kipindi cha miezi sita bila kuchanganyiwa maziwa ya mama na kitu kingine chochote

• Baada ya mtoto kunyonya kwa miezi sita maziwa ya mama pekee,anza kumchanganyia na vitu vingine lakini usiache kumnyonyesha maziwa ya mama mpaka afikishe umri wa miaka 2, Kumbuka maziwa ya mama ni kinga tosha dhidi ya magonjwa kwa mtoto wako, hasa katika kipindi cha miezi 3 ya mwanzoni ambapo kinga ya mtoto ipo chini sana

• Hakikisha mtoto anapata chanjo zote muhimu toka anazaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka 5

• Mahudhurio ya Kliniki ni Muhimu sana kwa mtoto wako, Na epuka kufanya vitu bila kuwauliza wataalam wa afya kuhusu afya ya mtoto wako.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments