Chanzo cha Mdomo Kuwa na Ladha ya Chumvi

Chanzo cha Mdomo Kuwa na Ladha ya Chumvi

Chanzo cha Mdomo Kuwa na Ladha ya Chumvi, Unatarajia mdomo wako kuwa na ladha ya chumvi baada ya kula chumvi au vyakula vyenye chumvi, Lakini ikiwa haujala halafu kinywa chako kina ladha ya chumvi, ni nini kinaendelea? 

CHANZO CHA TATIZO LA MDOMO KUWA NA LADHA YA CHUMVI 

Kwa nini mdomo wangu una ladha ya chumvi?

 Mara nyingi mtu kuwa na ladha ya chumvi kinywani sio tatizo ambalo huhitaji matibabu ya dharura yaani sio medical emergency

 - lakini pia hupaswi kupuuzia tatizo hili,lazima upate tiba. Baadhi ya Sababu za kinywa kuwa na ladha ya chumvi ni pamoja na: 

1. Upungufu wa Maji Mwilini yaani Dehydration Mate yako kwa asili yana kiasi kidogo cha chumvi. 

Lakini wakati una upungufu wa maji mwilini, chumvi kwenye mate yako inakuwa zaidi. Upungufu wa maji mwilini hubadilisha ubora wa mate yako ikiwemo ongezeko la chumvi kwenye mate yako, Mara nyingi, unaweza kuondoa ladha ya chumvi kwenye mdomo wako kwa kunywa maji ya kutosha kila siku. 

2. Kuwa na Tatizo la Mdomo mkavu(Dry mouth) au kwa kitaalam zaidi hujulikana kama xerostomia, Tatizo hili la mdomo kukauka hutokea wakati tezi zako za mate hazitengenezi mate ya kutosha. 

Watu wenye kinywa kikavu wanaweza kuona matatizo ya ladha pia, ikiwa ni pamoja na hili la kupata ladha ya chumvi mdomoni.

 3. Matumizi ya baadhi ya Dawa, baadhi ya dawa ukizitumia huweza kuwa na maudhi madogo madogo(side effects) kama vile;

 Kusababisha mdomo kukauka, kusababisha mdomo kuwa na Ladha ya chumvi n.k, Haya ni baadhi ya makundi ya dawa ambayo huweza kusababisha tatizo hili, 

• Dawa jamii ya Antidepressants hasa hasa tricyclic antidepressants.

 • Dawa jamii ya Antihistamines

 • Matibabu ya Chemotherapy kwa ajili ya Kansa

 • Dawa jamii ya Diuretics, hasa hasa zile zinazotolewa kwa wagonjwa wa moyo au Figo 

• Baadhi ya dawa za maumivu(Pain relievers)

 • Dawa jamii ya Sedatives, kwa ajili ya kutibu tatizo la wasiwasi(anxiety), panic disorders au matatizo ya Usingizi. 

4. Tatizo la Mzio(allergies) au maambukizi ya muda mrefu(sinus infection), ambayo husababisha ukavu mpaka kooni, Hii pia huweza kuleta ladha ya Chumvi mdomoni.

 5. Ujauzito, mabadiliko mengi hutokea kwa mjamzito kutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini, mabadiliko hayo ni pamoja na mama mjamzito kuvimba Pua, kupata sana hamu ya kula,kukosa kabsa hamu ya kula,na wakati mwingine kubadilika kabsa kwa ladha mdomoni ikiwemo kupata ladha ya Chumvi mdomoni. 

6. Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), Hii hutokea pale ambapo Acid kutoka tumboni hupanda juu kwenye esophagus, Tatizo hili huweza kubadilisha ladha mdomoni, na kuleta ladha ya Chumvi, ladha chungu(sour taste) n.k Pia watu wengi wenye tatizo hili la GERD (chronic acid reflux) hupata Kiungulia mara kwa mara, kikohozi ambacho hakiishi, na kuhisi kama kuna kitu kimebakia kooni. 

7. Tatizo la mfumo wa kinga Mwili(Autoimmune conditions), Hapa tunazungumzia wakati mfumo wa kinga yako ya mwili unapoanza kushambulia healthy tissue. Kama una matatizo kama vile lupus au rheumatoid arthritis, upo kwenye hatari zaidi ya kupata Sjögren’s syndrome. Hali ambayo huathiri tezi za Mate,na kusababisha Ukavu mdomoni pamoja na kubadilisha ladha mdomoni. 

8. Matatizo kwenye Neva(Neurological disorders), mabadliko yoyote yasioyakawaida kwenye ladha ikiwemo kupata ladha chungu au ladha ya chumvi mdomoni humaanisha kwamba sehemu ya Ubongo wako inayopokea taarifa zinazohusiana na ladha haifanyi kazi vizuri, 

Japo sio mara nyingi hutokea, lakini Nerves zinazohusishwa na kupeleka taarifa za ladha kwenye Ubongo zikiwa na shida yoyote kama vile; mtu akiwa na uvimbe kwenye ubongo,kuumia ubongo n.k, huweza kusababisha madhara mbali mbali ikiwemo; kubadilika kwa ladha mdomoni,maumivu ya kichwa,kizunguzungu,mtu kutokuona vizuri,kutokusikia harufu ya vitu n.k

 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584. 



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!