Ticker

6/recent/ticker-posts

Chanzo cha tatizo la Baridi Miguuni na Tiba yake



 Chanzo cha tatizo la Baridi Miguuni na Tiba yake

Unaweza kuhisi hali ya baridi sana miguuni,je unafahamu baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia hali hii?

1. Kipindi cha Baridi, Katika kipindi cha baridi ni kawaida sana kuhisi baridi miguuni,

Unapokuwa kwenye eneo lenye baridi zaidi, mishipa ya damu kwenye sehemu za mwisho, kama vile mikononi na miguuni, itabana. Hii inapunguza mtiririko wa damu kwenye maeneo haya, ambayo pia hupunguza kiasi cha joto ambacho mwili hupoteza.

Hali hii hupelekea maeneo haya kupoa zaidi au kuhisi baridi zaidi.

2. Kuwa kwenye Msongo wa Mawazo(Stress) au wasiwasi(Anxiety),

Kuwa katika hali ya msongo wa mawazo,mfadhaiko mkubwa au wasiwasi huweza pia kusababisha miguu kuwa ya baridi.

Mtu akiwa kwenye hali kama hii mwili huweza kusukuma adrenaline ndani ya damu.

Inapozunguka, adrenaline husababisha mishipa ya damu iliyo pembezoni kubana, ambayo hupunguza mtiririko wa damu hadi maeneo ya nje ya mwili. Hii husaidia Mwili kuhifadhi nishati na kujitayarisha kwa madhara yoyote ya mwili ambayo yanaweza kutokea, kutokana na hali ulionayo,

Lakini pia huweza kupelekea kuhisi hali ya baridi sana kwenye maeneo hayo.

3. Kwa ujumla kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu yaani Poor blood circulation kwenye maeneo haya huweza kuwa chanzo cha shida hii ya baridi,

Na poor blood circulation husababishwa na vitu vingi ikiwemo; Kukaa kwa muda mrefu(wale wanaofanya kazi za kukaa muda mrefu,siku nzima n.k), kunaweza kupunguza mzunguko wa damu kwenye miguu na kusababisha miguu kupata baridi.

4. Uvutaji wa tumbaku pia unaweza kuifanya iwe ngumu zaidi kwa damu kufikia kila eneo la mwili, kwa hivyo watu wanaovuta sigara wanaweza kulalamika shida hii miguu kuwa na baridi.

5. Cholesterol kuwa juu inaweza kusababisha uvimbe kutokea ndani ya ateri ambayo inaweza kupunguza mzunguko wa damu kwenye miguu, hivyo kusababisha baridi kwenye miguu.

6. Baadhi ya matatizo ya moyo yanaweza pia kusababisha miguu kuwa ya baridi, hivyo mtu anapaswa kufanyiwa vipimo vya moyo pia.

7. Upungufu wa damu au Anemia, Hali hii inatokea mtu anapokuwa na chembechembe nyekundu chache za damu katika mwili wake. Hii inaweza kutokana na sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na upungufu wa madini ya chuma, vitamini B12, au folate, au ugonjwa sugu wa figo.

Na baadhi ya watu wenye upungufu wa damu pia hulalamika miguu kuwa ya baridi.

8. Ugonjwa wa kisukari(Diabetes mellitus), Watu walio na kisukari wanaweza kuwa katika hatari ya matatizo ya mzunguko wa damu ikiwemo shida ya miguu kuwa ya baridi au mikono.

Shida ya sukari kuwa juu kwenye damu mara kwa mara huweza kusababisha kupungua(narrowing) kwa mishipa ya damu,hali ambayo huweza kupunguza mtiririko wa damu kwenye tishu, ambayo inaweza kusababisha miguu kuwa ya baridi.

Kwa baadhi ya watu, ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha tatizo la neuropathy , aina ya uharibifu wa neva ambao kwa kitaalam hujulikana kama diabetic peripheral neuropathy.

Matatizo haya ya neva yanaweza pia kusababisha Miguu kuwa na baridi sana.

9. Tatizo la Hypothyroidism ambalo hutokana na upungufu wa kiutendaji wa tezi yaani underactive thyroid gland, hali ambayo hupelekea upungufu kwenye uzalishwaji wa vichocheo ndani ya tezi la thyroid(thyroid hormones),

Tatizo hili huathiri mfumo wa kimetaboliki mwilini, mzunguko wa damu, mapigo ya moyo, joto la mwili n.k, hivyo chochote kinachoathiri utendaji wa tezi la thyroid na kusababisha hypothyroidism kinaweza kusababisha miguu kuwa ya baridi.

Watu walio na tatizo la hypothyroidism wanaweza kuathiriwa zaidi na baridi kwa ujumla, na wanaweza kupata dalili nyingine, kama vile  uchovu, kuongezeka uzito na matatizo ya kumbukumbu.

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUHISI BARIDI MIGUUNI

Tiba kubwa hutegemea na chanzo cha tatizo, kama nilivyokwisha kuelezea baadhi ya sababu hapo juu. Ila kwa ujumla zipo njia mbali mbali za kutatua tatizo hili ikiwemo Matumizi ya dawa mbali mbali kulingana na chanzo cha tatizo pamoja na kufanya vitu mbali mbali kama vile;

- Mtu kutokuaa sehemu moja kwa muda mrefu, hivo kuanza kutembea, kukimbia,au kufanya mazoezi

- Mtu kuvaa Soks Miguuni,

- Mtu kuweka miguu kwenye beseni lenye maji ya moto(Foot baths),loweka miguu kwa dakika 10 hadi 15 kunaweza kusaidia kuweka vizuri mzunguko wa damu miguuni. Hii inaweza kusaidia haswa kabla ya kulala, kwani inaweza pia kupunguza mvutano na kusaidia kupumzika kwa misuli.

Watu waliopata madhara zaidi kama uharibifu wa nerves n.k kutokana na kisukari wanapaswa kuepuka kutumia maji ya moto wakiwa pekee yao kwa lengo la kusaidia miguu kupata joto kama nilivyoelezea hapo, kwa kuwa hawawezi kujua ikiwa maji ni moto sana au la. Hii inaweza kusababisha kuchoma miguu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments