CHANZO CHA TATIZO LA WATOTO KUFIA TUMBONI

 CHANZO CHA TATIZO LA WATOTO KUFIA TUMBONI

Moja ya matatizo ambayo huweza kutokea kipindi cha ujauzito ni pamoja na mimba kutoka zenyewe au mtoto kufia tumboni na kutofautisha hivi vitu viwili soma maelekezo hapa chini,

Ujauzito kutoka mara nyingi hutokea kwenye miezi ya mwanzoni kama miezi 3 yaani First Trimester n.k na huhusisha kiumbe kutoka nje lakini swala la mtoto kufia tumboni linahusisha kiumbe kufia ndani ya tumbo la uzazi yaani Intrauterine death kabla ya kutoka nje na huweza kujumuisha vipindi mbali mbali vya ujauzito mfano; ujauzito ukiwa na wiki 20,28 n.k

CHANZO CHA TATIZO LA WATOTO KUFIA TUMBONI WAKATI WA UJAUZITO

Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili kwa wakina mama wajawazito,na sababu hizo ni kama vile;

- Mtoto mwenyewe kuwa na matatizo kwenye uumbaji wake yaani Congenital birth defects

- Matatizo ya vinasaba au Genetic abnormalities

- Matatizo kwenye kondo la nyuma la uzazi yaani Placenta, kama vile; tatizo la kondo la nyuma kuachia sehemu lilipojishikiza ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Placental abruption pamoja na matatizo mengine kwenye placenta kama vile tatizo la vasa previa n.k

- Kondo la nyuma kutokufanya kazi vizuri yaani Placental dysfunction hali ambayo husababisha mtoto kukosa virutubisho vya kutosha pamoja na hewa safi ya oxygen kitu ambacho huathiri kwa kiasi kikubwa sana ukuaji wa mtoto hata kuweza kupelekea tatizo la mtoto kufia tumboni

- Wakati mwingine Kondo la nyuma(Placenta) halina matatizo yoyote lakini shida ikatokea kwenye ile kamba ambayo huunganisha placenta pamoja na mtoto yaani Umbilical cord complications, hapa tunazungumzia matatizo mbali mbali kama; ile kamba(umbilical cord) kubanwa sana na kushindwa kusafirisha damu, tatizo la cord kujizungusha yenyewe, tatizo la cord kumnyonga mtoto shingoni n.k

- Sababu nyingine ya watoto kufia tumboni ni pamoja na tumbo la uzazi kupasuka ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Uterine rupture.

KUNDI LA WAKINA MAMA AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI LA WATOTO KUFIA TUMBONI WAKATI WA UJAUZITO NI PAMOJA NA;

1. Wakina mama wajawazito wenye matatizo ya kiafya kama vile; tatizo la Presha,ugonjwa wa kisukari,Lupus,Magonjwa ya Figo,matatizo kwenye tezi la thyroid,matatizo kwenye damu kama vile thrombophilia n.k

2. Wakina mama wanaovuta Sigara kipindi cha ujauzito

3. Wakina mama wanaokunywa pombe kipindi cha ujauzito

4. Wakina mama wajawazito ambao ni wanene kupita kiasi au wenye tatizo la obesity

5. Wakina mama wanaochelewa sana kubeba mimba mfano kwa zaidi ya miaka 35

6. Wakina mama wenye watoto zaidi ya mmoja tumboni N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!