DALILI ZA FIGO KUJAA MAJI NA DAWA YAKE
Tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama HYDRONEPHROSIS,ambapo hutokea pale ambapo figo zako zinakuwa na kiwango kikubwa cha maji yaani Excess Fluid kutokana na kujaa kwa Mkojo,
Mara nyingi chanzo chake ni kuziba kwa njia ya mkojo yaani upper part of Urinary tract(ureters) ambayo hutoa mkojo kwenye figo,
Au wakati mwingine huweza kuhusishwa na Anatomical Defects ambayo hairuhusu mkojo kutoka vizuri,
Figo kujaa maji ni tatizo ambalo huhusisha figo kuvimba kutokana na mkojo kushindwa kutoka nje ya Figo,
Shida hii huweza kutokea kwa mtu mwenye umri wowote, na kwa watoto wadogo wanaweza kugunduliwa baada ya kuzaliwa au hata mtoto akiwa tumboni kwa kutumia kipimo cha Ultrasound yaani Prenatal Ultrasound,
DALILI ZA FIGO KUJAA MAJI NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kupata maumivu upande mmoja na mgongoni ambayo husambaa mpaka chini ya tumbo au kwenye sehemu za siri
- Mgonjwa kupata matatizo mbali mbali wakati wa kukojoa, kama vile maumivu wakati wa kukojoa, au mgonjwa kuhisi mkojo kila mara ndani ya muda mfupi sana
- Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika
- Mgonjwa kupata homa au joto la mwili kuwa juu zaidi
- Mwili kukosa nguvu au mgonjwa kuchoka sana n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Njia ya Mkojo kuziba, Mara nyingi chanzo chake ni kuziba kwa njia ya mkojo yaani upper part of Urinary tract(ureters) ambayo hutoa mkojo kwenye figo,
- Au wakati mwingine huweza kuhusishwa na Anatomical Defects ambayo hairuhusu mkojo kutoka vizuri
- Shida ya mkojo kurudi wenyewe kwenye figo(Urine backups) au shida ya mkojo kubakia ndani ya Figo(Kidney) au kwenye Njia ya mkojo(Ureter)
- Tatizo la Vesicoureteral reflux, Shida hii hutokea pale ambapo; mkojo unarudi kupitia njia yake(ureter) kutoka kwenye kibofu cha mkojo kupanda juu kwenye Figo,
- Kwa kawaida mkojo husafiri kwenye muelekeo mmoja tu yaani one way direction, Hivo hali ya mkojo kupitia njia ambazo sio sahihi husababisha iwe vigumu sana figo kutoa mkojo vizuri na kupelekea Figo zako kuvimba
VIPIMO VYA KUFANYA NI PAMOJA NA;
- Blood tests-Ili kuchunguza utendaji kazi wa figo zako
- Urine test- Ili kuchunguza uwepo wa maambukizi kwenye njia ya mkojo au shida ya mawe yaani Urine stones ambayo huweza kuziba njia ya Mkojo
- Vipimo vya ULTRASOUND
- Specialized X-Ray n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI(DAWA YA TATIZO HILI LA FIGO KUJAA MAJI)
-Endapo tatizo hili sio kubwa sana yaani Mild or moderate HYDRONEPHROSIS,mgonjwa huweza kupona mwenyewe bila matibabu makubwa, hapa Mgonjwa huweza kupewa tu Preventive Antibiotics za UTI
- Endapo tatizo ni kubwa sana yaani Severe HYDRONEPHROSIS mgonjwa huweza kupewa matibabu kama vile UPASUAJI na kuondoa hiyo blockage au kurekebisha palipoziba.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!