Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito

Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito.

Fahamu Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito,Kupitia Makala hii,

Habari! Karibu kwenye tovuti yetu ambapo tunajitahidi kuwaelimisha wanawake kuhusu afya ya uzazi. Leo, tutakuwa tukijadili dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito.

Katika kipindi hiki, mwili wa mama huwa unapitia mabadiliko mengi sana, na ni muhimu sana kujua kuhusu dalili za mimba changa ili kuweza kuhakikisha afya ya mama na mtoto inakuwa Salama wakati wote.

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za mimba changa;

1. Kuchoka sana:

Mwili wa mama unapotumia nguvu zake(energy) nyingi kwa ajili ya ukuaji wa mtoto, ni kawaida kwa mama kujisikia uchovu sana kuliko kawaida,

Hivo hali hii ni miongoni mwa Dalili za mimba changa.

2. Kuhisi kichefuchefu:

Kichefuchefu kinaweza kutokea wakati wowote wa siku, lakini mara nyingi hutokea asubuhi,

Hii ni kutokana na kuongezeka kwa vichocheo au hormones wakati wa ujauzito ambazo hupunguza mwendo wa chakula tumboni yaani food movement,

hivo basi, kuhisi kichefuchefu ni mojawapo ya Dalili za mimba changa.

3. Kutapika:

Kutapika pia ni dalili nyingine ya mimba changa, ingawa si kila mama mjamzito anatapika.

4. Kukojoa mara kwa mara:

Kukojoa mara kwa mara ni kawaida wakati wa ujauzito, kwa sababu ya kuongezeka kwa uzalishaji wa damu pamoja na vichocheo mbali mbali,

Hivo basi, hii pia huweza kuwa mojawapo ya Dalili za mimba changa,

ingawa hata baada ya Ujauzito kuendelea kukua hali hii huweza kuzidi kwasababu kadri mtoto anavyokua tumboni huongeza mgandamizo(pressure) kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha kupungua zaidi kwa nafasi ya kutunza mkojo ndani ya kibofu(urinary bladder room).

5. Kuvimba kwa matiti:

Matiti ya mama yanaweza kuvimba na kuwa na maumivu kutokana na mabadiliko ya hormones kipindi cha ujauzito.

Pia hali ya weusi zaidi kuongekeza kwenye eneo la Chuchu.

Mabadiliko yote haya huweza kuwa Dalili za mimba changa.

6. Kuhisi baridi au joto kali:

Mama anaweza kuhisi baridi au joto kali wakati wa mimba changa kutokana na mabadiliko ya hormones au vichocheo kipindi cha ujauzito.

7. Kupata maumivu ya kichwa:

Kupata maumivu ya kichwa wakati wa mimba changa ni kawaida, lakini ni muhimu kuwa na tahadhari ikiwa maumivu ni makali sana.

8. Kuongezeka kwa hisia dhidi ya harufu:

Mama anaweza kuhisi harufu kali sana wakati wa mimba changa, hata kwa harufu ambazo hapo awali hazikuwa na nguvu sana.

Hivo hii pia ni mojawapo ya Dalili za mimba changa.

10. Kukosa hamu ya kula:

Kupungua kwa hamu ya kula ni dalili nyingine ya mimba changa, ingawa kila mama mjamzito hupata uzoefu tofauti.

11. Kupata hamu ya kula kitu maalum:

Kupata hamu ya kula kitu maalum ni dalili nyingine ya mimba changa

12. Kuvimba kwa mwili:

Mama anaweza kuvimba sehemu tofauti za mwili wake, kama vile miguu, mikono na uso, Japo wakati mwingine kuvimba sana miguu,mikono na uso huweza kuwa dalili za matatizo kama vile Kifafa cha Mimba.

13. Kupata upele:

Mama anaweza kupata upele au kuchubuka ngozi wakati wa mimba changa kutokana na mabadiliko ya homoni.

14. Kusikia maumivu ya mgongo:

Maumivu ya mgongo ni kawaida wakati wa mimba changa kutokana na kuongezeka kwa uzito wa mama na mtoto.

15. Kupata mafua:

Kupata mafua ni kawaida wakati wa mimba changa kutokana na mfumo wa kinga ya mwili wa mama kuwa dhaifu kidogo.

16. Kupata vidonda mdomoni:

Vidonda mdomoni ni kawaida wakati wa mimba changa kutokana na mabadiliko ya homoni na upungufu wa madini fulani mwilini.

17. Kupata maumivu ya kifua:

Maumivu ya kifua ni kawaida wakati wa mimba changa kutokana na shinikizo la mtoto kwenye mfumo wa moyo.

18. Kupata maumivu ya tumbo:

Maumivu ya tumbo yanaweza kutokea wakati wa mimba changa kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto.

19. Kupata tatizo la kuharisha:

Mama anaweza kupata tatizo la kuharisha wakati wa mimba changa kutokana na mabadiliko ya homoni na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kuwa dhaifu kidogo.

20. Kupata matatizo ya usingizi:

Kupata tatizo la usingizi au kukosa usingizi ni kawaida wakati wa mimba changa kutokana na mabadiliko ya homoni na mabadiliko ya mwili.

Hizo ni baadhi ya Dalili za mimba changa, endelea zaidi hapa..!!!

• SOMA ZAIDI Hapa,Kuhusu Dalili za Mimba Changa

DALILI ZA MWANZO ZA MIMBA CHANGA

Hizi hapa ni baadhi ya dalili za Mwanamke mjamzito au mwanamke mwenye mimba,Dalili hizi ni toka mimba imetungwa mpaka inapokuwa kubwa.

1. Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi(Kumiss period)

2. Mwanamke kutema mate sana mara kwa mara

3. Matiti kuuma pamoja na kujaa

4. Kuhisi hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwa mara

5. Kukojoa mara kwa mara

6. kupata uchovu wa mwili kupita kiasi

7. Mapigo ya moyo kwenda mbio

8. Kuwa mtu wa kukasirika mara kwa mara kwa baadhi ya Wanawake

9. Tumbo kujaa mithili ya kuwa na Gesi

10. Tumbo kukaza na kuvuta

11. Kupata vidamu vidamu kidogo yaani Light spot, na hii hutokea wakati mtoto anajishikiza kwenye mji wa uzazi

12. Kuanza kupata choo kigumu mara kwa mara yaani constipation

13. Kuvimba pua, hii hutokana na mabadiliko ya vichocheo pamoja na mzunguko wa damu hali ambayo hupelekea kuvimba kwa Mucous membrane puani

14. Kubadilika ngozi ya mwili hasa maeneo ya usoni, na kuwa na vitu vyeupe tofauti na rangi ya kawaida ya ngozi

15. Kuanza kupata kiungulia mara kwa mara

16. Kukosa usingizi

17. Kubadilika mfumo wa kula, na kuanza kupenda baadhi ya vyakula na kuchukia baadhi ya vyakula

18. Kuanza kupenda harufu za vitu flani na kuanza kuchukia harufu za baadhi ya vitu

19. Kupenda kula mara kwa mara

20. Kutapika mara kwa mara baada ya kula chakula

N.k

Hitimisho

Hizo ndyo baadhi ya Dalili za mimba changa,

Ni muhimu kuelewa kuwa dalili hizi hazitokei kwa kila mama mjamzito, na kwamba zinaweza kutokea kwa kiwango tofauti kwa kila mjamzito. Kama una wasiwasi wowote kuhusu dalili unazopata, unapaswa kuzungumza na daktari wako au mtaalamu wa afya.

Kwa sababu ya umuhimu wa kujua dalili za mimba changa, tunapendekeza kuwa mama anapaswa kufuatilia kwa karibu dalili zake, na kupata msaada wa kitaalamu ikiwa ana wasiwasi wowote.

Asanteni kwa kutembelea tovuti yetu na tunatumai kuwa umejifunza kitu kipya kuhusu dalili za mimba changa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!