Ticker

6/recent/ticker-posts

DAMU KUWA NYINGI MWILINI,CHANZO,DALILI NA TIBA



DAMU KUWA NYINGI MWILINI,CHANZO,DALILI NA TIBA

Tatizo la damu kuwa nyingi mwilini au damu kuzidi hujulikana kama Polycythemia, hapa huhusisha kuongezeka kwa idadi ya seli nyekundu za damu yaani red blood cells(RBC's) mwilini.

Seli hizi zikizidi husababisha Damu kuwa nzito hali ambayo huweza kupelekea matatizo mengine kama vile damu kutengeneza Clots n.k

AU, Damu kuwa nyingi huhusisha kiwango cha haemoglobin kuwa kikubwa kuliko kawaida, mfano;

Kwa mtu mzima Mwanaume akiwa na kiwango cha zaidi ya haemoglobin 16.5g/dL na Mtu mzima mwanamke akiwa na kiwango cha zaidi ya haemoglobin 16g/dL basi wanaweza kuwa kwenye kundi la watu wenye damu nyingi mwilini.

CHANZO CHA DAMU KUWA NYINGI MWILINI

Kuna sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia tatizo hili la damu kuzidi mwilini na matibabu yake hutegemea sababu hizi.

Sababu hizi zipo kwenye makundi makubwa mawili yaani Primary polycythemia na Secondary polycythemia

1. Primary polycythemia au kwa jina lingine hujulikana kama polycythemia vera (PV).

- Aina hii ni mara chache sana kutokea, na hii huhusisha kansa ya damu ambayo huanza taratibu sana, na kitaalam hujulikana kama myeloproliferative neoplasm.

Kansa hii(polycythemia vera), husababisha bone marrow kutengeneza blood cells nyingi zaidi ambazo hufanya kazi isivyokawaida, hali ambayo huchangia kuzalishwa kwa wingi sana kwa seli nyekundu za damu yaani Red blood cells-RBC's.

Lakini pia mtu mwenye kansa hii(polycythemia vera) huweza kupata ongezeko la Seli nyingine za damu kama vile white blood cells au platelets.

2. Secondary polycythemia,

Hii ni aina ya ongezeko la damu mwilini ambayo huchangiwa na sababu zingine mbali na kansa(polycythemia vera) au myeloproliferative disease.

Na kwenye kundi hili, ndyo kuna idadi kubwa ya watu hupata shida ya damu kuwa nyingi mwilini.

SABABU HIZO AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA DAMU KUWA NYINGI MWILINI NI PAMOJA NA;

- Kubadilisha mazingira na kwenda sehemu zenye mwinuko zaidi(very high altitude),

Mfano; nimetoka Dodoma nikaenda kukaa Mbeya,

- Kuwa na tatizo la obstructive sleep apnea

- Kuwa na aina mbali mbali za tumor

- Kuwa na magonjwa ya moyo au mapafu ambayo husababisha upungufu wa Oxygen mwilini.

- Mtindo wa maisha ikiwemo vyakula tunavyokula

- Matumizi ya dawa za kuongeza Damu mwilini N.k

DALILI ZA DAMU KUWA NYINGI MWILINI NI PAMOJA NA;

• Mtu kuanza kupata kizunguzungu

• Kupata maumivu makali ya kichwa

• Mwili Kutoa jasho sana kupita kawaida

• Kuanza kupata miwasho kwenye ngozi(itchy skin)

• Kusikia sauti masikioni ambazo hujulikana kama ringing

• Mtu kuanza kuona marue rue(blurred vision)

• Kupata uchovu wa mwili kupita kawaida

• Ngozi ya kwenye viganja vya mikono,puani,n.k kuwa nyekundu zaidi

• Kuumia kidogo kuvuja damu nyingi

• Kuhisi hali ya kuchomwa chomwa chini ya miguu

• Kuvuja damu puani mara kwa mara(Nose bleeding)

• Kuvuja damu kwenye Fizi mara kwa mara(Gum bleeding) N.K

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA ILI KUJUA WINGI WA DAMU PAMOJA NA CHANZO CHAKE

- Blood tests

- Bone marrow biopsy

- Genetic tests N.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA DAMU KUWA NYINGI MWILINI

kama nilivyokwisha kusema,Matibabu yake hutegemea na chanzo chake, lakini kwa ujumla zipo njia mbali mbali ambazo huweza kutumika kama vile;

• Kubadilisha mtindo wa maisha ikiwemo vyakula unavyokula

• Epuka uvutaji wa Sigara

• Epuka kukaa sehemu ambazo kuna kiwango kikubwa cha hewa ya carbonidioxide kama vile viwandani,kwenye machimbo n.k

• Epuka kukaa maeneo ambayo ni high altitude

• Pata matibabu ya magonjwa kama vile; magonjwa ya moyo,mapafu n.k

• Dawa za kudhibiti utengenezwaji wa Blood cells kama zile za kuzuia Bone marrow mfano hydroxyurea (Hydrea) n.k

• Dawa za kudhibiti dalili zote zitokanazo na damu kuzidi mwilini, kama vile Asprin ambazo huweza kusaidia kuzuia blood clots n.k





Post a Comment

0 Comments