Ticker

6/recent/ticker-posts

DAWA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KUTUMIA MAMA MJAMZITO



 DAWA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KUTUMIA MAMA MJAMZITO

Kuna dawa nyingi ambazo haziruhusiwi kwa matumizi ya mama mjamzito hasa katika miezi mitatu(3) ya mwanzo yaani first trimester ambapo uumbaji wa viungo mbali mbali vya mtoto aliyetumboni hufanyika.

Hivo zifuatazo ni baadhi ya dawa ambazo huweza kuongeza uwezakano wa mtoto kupata matatizo kwenye uumbaji wake na mama mjamzito anashauriwa kutokutumia kabsa au kutumia baadhi ya dawa hizi kwa maelekezo ya kina na uangalizi wa karibu kutoka kwa wataalam wa afya pale ambapo hakuna mbadala wake;

1. Dawa za maumivu jamii ya Asprin pamoja na Ibuprofen(Motrin,Advil)

2. Dawa jamii ya Isotretinoin ambapo mwanzoni zilikuwa zinajulikana kwa jina la Accutane

3. Thalidomide ambayo hutumika kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali ya ngozi pamoja na tatizo la multiple myeloma

4. Albendazole za minyoo,badala yake mama mjamzito hushauriwa kutumia mebendazole pale afikapo kliniki

5. Dawa jamii ya Bismuth subsalicylate kama vile Pepto-Bismol n.k

6. Dawa jamii ya phenylephrine

7. Dawa za mafua na kikohozi ambazo ndani yake zina Guaifenesin

8. Dawa jamii ya ACE inhibitors kama vile Benazepril pamoja na Lisinopril

9. Baadhi ya dawa kwa ajili ya kudhibiti hali ya mtu kutetemeka mwili(Seizures) mfano kwa mgonjwa wa kifafa cha mimba, dawa hizo ni kama vile Valproic acid haziruhusiwi kutumika kabsa

10. Baadhi ya dawa jamii ya viuwajivisimu(antibiotics) kama vile Doxycycline pamoja na Tetracycline

11. Dawa za methotrexate ambazo kuna muda hutumika kwa ajili ya tatizo la arthritis

12. Dawa jamii ya Warfarin kama vile coumadin

13. Dawa za lithium ambazo hutumika kutibu tatizo la Bipolar depression

14. Dawa jamii ya Alprazolam kama vile Xanax,Diazepam mfano wa valium n.k

15. Dawa jamii ya Paroxetine kama vile paxil ambazo hutumika kwa watu wenye matatizo ya depression pamoja na matatizo mengine

16. Matumizi ya dawa jamii ya Chloramphenicol huweza kusababisha matatizo kwenye damu pamoja na tatizo la mtoto kuzaliwa na shida ya Gray baby syndrome

17. Matumizi ya ciproflaxin maarufu kama Cipro kwa magonjwa mbali mbali kama vile UTI pamoja na Matumizi ya dawa za Levofloxacin

18. Matumizi ya dawa za Primaquine ambazo hutumika kutibu ugonjwa wa Malaria

19. Sulfonamides ikiwa na maana ya antibiotics au dawa zote zenye sulfa ndani yake

20. Matumizi ya antibiotics za Trimethopram(primsol) huweza kusababisha hitilafu kwa mtoto ambayo hujulikana kama neural tube defects

21. Matumizi ya Codeine kwa ajili ya kuondoa maumivu huweza kusababisha shida ya withdrawal symptoms kwa mtoto

22. Matumizi ya Lorazepam kwa ajili ya kutibu tatizo la wasi wasi au Anxiety disorders pamoja na matatizo mengine yanayohusu afya ya akili

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments