Ticker

6/recent/ticker-posts

DAWA YA UGONJWA WA UTI(kwa wanaume na wanawake)



DAWA YA UGONJWA WA UTI(kwa wanaume na wanawake)

Ugonjwa wa uti-Urinary track infection au maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo ikiwemo ni pamoja na kibofu cha mkojo,Figo,Njia ya Mkojo N.K 

Ugonjwa huu huwashambulia sana wanawake mara kwa mara hata zaidi ya wanaume,ikiwemo ni pamoja na sababu mbali mbali kama za kimaumbile,hali kama ya ujauzito ambayo hushusha kinga ya mwili na kuufanya mwili kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama UTI,fangasi,PID N.K

DAWA YA UGONJWA WA UTI 

Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika hospitalin kutibu ugonjwa huu wa UTI na dawa hizo ni pamoja na;

1. Azuma au Azthromycin ambapo vinakuwa vidonge vitatu kama dose, na mtu humeza kidonge kimoja kimoja ndani ya siku tatu yaani 1×1 kwa siku 3.

2. Ciproflaxin hii pia ni dawa nzuri ambayo hutumika hospitalin kutibu ugonjwa huu wa UTI

3. Amoxicillin, hii ni dawa nzuri kwa kutibu ugonjwa wa UTI hasa hasa kwa wakina Mama wajawazito kwani hawatakiwi kutumia dawa kali ambazo huweza kuleta madhara mbali mbali kwenye ujauzito wao.

ANGALIZO; Ni marufuku na ni hatari pia kutumia dawa hovio pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya juu ya aina ya dawa sahihi kwako kwa kuzingatia sababu mbali mbali kama afya ya mwili wako,kinga yako ya mwili,allegy za dawa N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments