Gharama za kipimo cha mri Tanzania
Kipimo cha MRI
Kipimo cha MRI,Fahamu mambo mbali mbali kuhusu kipimo cha MRI,Kupitia kwenye Makala hii ikiwemo Gharama za kipimo cha mri Tanzania.
FAHAMU MAMBO MBALI MBALI KUHUSU KIPIMO YA MRI IKIWEMO Gharama za kipimo cha mri Tanzania.
Bila shaka neno MRI sio geni kwako na kwa namna moja au nyingine umewahi kusikia mtu akisema mgonjwa kaambiwa afanyiwe kipimo cha MRI,
japo unaweza usielewe hicho kipimo cha MRI ni nini na kinafanya kazi gani,karibu hapa ujifunze na upate kuelewa kuhusu kipimo cha MRI.
MRI-kirefu chake ni "Magnetic resonance imaging", yaani ni aina ya mashine ambayo hutumia Sumaku kuscan au kupiga picha mwili wako kisha kutoa majibu wapi kuna tatizo,
Kipimo cha MRI kinaweza kuchunguza maeneo gani?
kipimo cha MRI huweza kuchunguza karibia kila sehemu kwenye mwili wako na kugundua tatizo lipo wapi,
sehemu Mbali mbali za mwili ambazo kipimo cha MRI kinaweza kuchunguza ni pamoja na;
- Maeneo ya kichwani ikiwemo pamoja na Ubongo mzima
- Maeneo ya kwenye uti wa mgongo
- Maeneo ya kwenye mifupa pamoja na joints zote
- Maeneo ya moyo pamoja na Mishipa ya damu
- Maeneo ya kwenye matiti
- Viungo vya ndani kama vile Ini,Tumbo la uzazi yaani womb/uterus, tezi la Prostate n.k
Gharama za kipimo cha mri Tanzania
Yapo maswali mengi kuhusu Gharama za kipimo cha mri Tanzania,huku Watu mbali mbali wakihitaji kufahamu zaidi kuhusu gharama za kipimo hiki cha MRI kwa hapa kwetu Tanzania,
Zipo Comments mbali mbali za watu kwenye Jukwaa Maarufu la Midahalo Tanzania,Jamiiforum wakitoa maswali na majibu kuhusu Gharama za kipimo cha mri Tanzania,
Mfano;Wapo baadhi walisema,Gharama za kipimo cha mri Tanzania ni Laki 3(300,000) kwa upande wa Brain MRI kwa MOI,wengine Zaidi ya Laki 3 kulingana na vipimo unavyohitaji kufanya na MAHALI unapofanyia Vipimo vyako n.k
Hizi ni baadhi ya Comments za June 16,2021
Ingawa kadri siku zinavyozidi kwenda Gharama za kipimo cha mri Tanzania hupungua Zaidi, na Upatikanaji wa Vipimo hivi vya MRI kwenye hospital Zetu unaongezeka Zaidi.
Hii ina maana Gharama za kipimo cha mri Tanzania mwaka 2021 sio sawa na Gharama za kipimo cha mri Tanzania mwaka 2023.
Upimaji kwenye Kipimo cha MRI
JINSI MGONJWA ANAVYOPIMWA KWENYE KIPIMO CHA MRI
Mgonjwa hulala chali kwenye kitanda cha mashine ya MRI huku akiwa katanguliza kichwa au miguu kulingana na kitu gani kinatakiwa kuchunguzwa kwanza,
kisha kitanda chenyewe husogea na kumpitisha mgonjwa kwenye mashine kwa ajili ya kuchunguzwa maeneo mbali mbali ya mwili wake,
Zoezi hili huweza kuchukua muda wa dakika 15 na kuendelea kulingana na ukubwa wa tatizo na idadi ya picha ambazo huhitajika kuchukuliwa kutoka kwa mgonjwa.
JINSI KIPIMO CHA MRI KINAVYOFANYA KAZI
Mwili wa binadamu umetengenezwa kwa kiasi kikubwa cha Molecules za maji ambazo hujumuisha atoms za hydrogen pamoja na Oxygen,
Katikati ya kila atom moja ya hydrogen kuna particle ndogo ambazo huitwa proton.
Hizi Protons ni kama visumaku vidogo sana, hivo hupokea hisia kwa haraka sana baada ya kupitishwa kwenye mashine yenye sumaku kama MRI,
Na wataalam husema wakati umelala kwenye mashine ya MRI zile protons hujipanga kwenye mstari mmoja kama vile sumaku ikivuta sindano au kitu chochote chenye asili ya chuma,
hivo kitendo hiki husababisha kutengenezwa kwa mawimbi yaani radio waves ambayo hutumwa moja kwa moja kwenye maeneo mbali mbali kwenye mwili wako kisha kukutana na protons ambazo zimejipanga kwenye direction moja,
Na hapa ndipo taarifa kuhusu maeneo mbali mbali ya mwili wako hutumwa na kupokelewa na kifaa ambacho kipo kwenye mashine ya MRI kinachojulikana kama RECEIVER,
taarifa hizo husaidia kujua maeneo sahihi ambapo protons kwenye mwili wako zipo,kusaidia kutofautisha aina mbali mbali za tissue kwenye mwili wako, pamoja na kutoa taarifa kuhusu wapi kuna tatizo kwenye mwili wako.
JE KIPIMO CHA MRI NI SALAMA?
Mbali na watu kuhitaji zaidi kufahamu Gharama za kipimo cha mri Tanzania,yapo baadhi ya Maswali mengi kuhusu Usalama wa kipimo cha MRI,
Kipimo cha MRI ni salama na wala hakisababishi maumivu yoyote kwenye mwili wako,
japo kwa mgonjwa mwenye matatizo kama Caustrophobia anaweza asijisikie comfortable,
Tafiti mbali mbali zinaendelea kufanyika duniani kote kuhusu usalama wa mashine ya MRI na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kuhusu madhara ya Kipimo cha MRI,
Japo kipimo cha MRI hakiruhusiwi kufanyika kwa baadhi ya makundi ya watu kama vile;
- Wagonjwa waliowekewa kifaa cha PACEMAKER
- Wagonjwa waliowekewa joints za bandia yaani artificial joint
- Na pia kipimo cha MRI hakiruhusiwi kwa mama mjamzito
•Soma Zaidi hapa Pia,Kuhusu Kipimo cha MRI,na jinsi kinavyofanya kazi
Hitimisho
Ni muhimu kujua au kufahamu kuhusu Gharama za kipimo cha mri Tanzania, ili endapo itahitajika kufanya Kipimo cha MRI uweze kujiandaa,
Lakini pia ni muhimu kufahamu kuhusu kipimo chenyewe cha MRI,jinsi kinavyofanya kazi, faida zake,watu gani hawawezi kufanya kipimo cha MRI N.k
Asante kwa Kusoma na kufahamu mambo mbali mbali kuhusu kipimo cha MRI.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!