Gharama za kusafisha figo kupunguzwa
Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) inafanya jitihada za kununua vitendanishi na vifaa vinavyotumika kusafisha figo moja kwa moja kutoka Viwandani ili kupunguza gharama za huduma hiyo.
Hayo yamesemwa leo Agosti 27, 2024 na Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.
Aidha Dkt. Mollel amesema serikali imeanza kuchukua hatua katika kupunguza gharama za matibabu kwani kwa Hospitali ya Temeke gharama zimeshuka hadi laki moja na nusu.
Pia, Dkt Mollel ametoa rai kwa wananchi mara utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote utakapoanza waweze kujiunga kwani ni njia pekee ya kuweza kuwasaidia kuepuka gharama za matibabu.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!