Homa ya Nyani yatangazwa kuwa dharura ya kiafya barani Afrika
Homa ya Nyani, ugonjwa hatari wa kuambukiza ambao ulikuwa ukiitwa Mpox, umetangazwa kuwa dharura ya kiafya ya umma barani Afrika na bodi kuu ya afya ya bara hilo.
Wanasayansi kutoka Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) wanasema wanasikitishwa na kasi ambayo maambukizi mapya ya mpox yamekuwa yakienea.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, zaidi ya kesi 13,700 na vifo 450 vimerekodiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Virusi hivyo vinavyoweza kusababisha vidonda katika mwili mzima vimesambaa hadi katika mataifa mengine ya Afrika, ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Kenya na Rwanda.
Mpox ni nini na inaeneaje?
Tangazo la dharura ya afya ya umma litasaidia serikali kuratibu majibu yao na uwezekano wa kuongeza usambazaji wa vifaa vya matibabu na misaada katika maeneo yaliyoathirika.
Wakuu wa afya nje ya Afrika pia watakuwa wakifuatilia hali hiyo ili kutathmini hatari ya mlipuko huo kuenea zaidi.
Homa ya Nyani huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu na kati ya watu kwa kuwasiliana kwa karibu na mtu aliyeambukizwa – ikiwa ni pamoja na ngono, kugusana kwa ngozi hadi ngozi na kuzungumza au kupumua karibu na mtu mwingine.
Inaweza kusababisha dalili kama vile homa, maumivu ya misuli na vidonda kwenye mwili.
Ikiachwa bila kutibiwa, mpox inaweza kuwa hatari.Kuna aina mbili kuu za virusi vinavyojiulikana kuwepo.
Hali mbaya zaidi ilisababisha mlipuko wa kimataifa mnamo 2022 ambao uliathiri bara Uropa, Australia, Marekani na nchi zingine nyingi – na ulienezwa haswa kupitia mawasiliano ya ngono.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!