MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA
Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo cha tatizo la maumivu makali ya njia ya haja kubwa ni Bawasiri,ila sio kila mtu mwenye maumivu makali sehemu ya njia ya haja kubwa basi ana Bawasiri.
Baada ya kuliona hilo na kukutana na maswali mengi juu ya tatizo hili la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la bawasiri,nmeona nitoe maelekezo kwa kina kuhusu baadhi ya sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kupatwa na tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa ambayo huweza kutokea wakati anajisaidia au hata akiwa amekaa tu.
Sababu au Chanzo cha Maumivu makali sehemu ya Haja Kubwa
BAADHI YA SABABU ZA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA NI PAMOJA NA;
1. Tatizo la Bawasiri,kutoka kinyama sehemu ya haja kubwa,kuvimba kwa mishipa ya vein kwenye njia ya haja kubwa, hapa kuna bawasiri ya ndani pamoja na bawasiri ya nje,zote hizi huweza kusababisha maumivu makali ya sehemu ya haja kubwa
2. Mtu Kuwa na tatizo la jipu au majipu ambayo yametokea kwenye njia ya haja kubwa
3. Uwepo wa tatizo la Saratani au Kansa ya sehemu ya haja kubwa kama vile;Anal cancer,Rectum cancer n.k
4. Mtu kupatwa na tatizo la Fistula ambalo hujulikana kama Anal fistula
5. Mtu kupatwa na majeraha yoyote au michubuko kwenye sehemu ya haja kubwa,kutokana na sababu mbali mbali kama vile; kufanya mapenzi kinyume na maumbile yaani Anal sex, kuumia kwenye ajali n.k
6. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria,Fangasi, Virusi,Minyoo n.k
7. Maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya zinaa yaani sexual transmitted infections(STD's)
8. Magonjwa kama Crohn's, ambapo huu ni ugonjwa ambao huhusisha mtu kuvimba utumbo au kuwa na vidonda ambavyo huweza kuwepo kwenye utumbo lakini pia kwenye Rectum hata kupelekea mtu kuharisha au kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na Damu
9. Tatizo la Levator Ani syndrome, ambapo misuli ya sehemu ya haja kubwa huwa dhaifu,kukakamaa,ukavu kupita kawaida,hali ambayo huleta maumivu ya njia ya haja kubwa hasa wakati wa kujisaidia
10. Tatizo la Pelvic Floor Dysfunction,ambapo misuli kwenye eneo lote la nyonga ikiwa ni pamoja na sehemu ya haja kubwa kushindwa kutanuka vizuri
11. Magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile; Psoriasis, maambukizi ya fangasi kwenye njia ya haja kubwa n.k
12. Tatizo la mtu kujisaidia kinyesi kigumu au kwa kitaalam hujulikana kama Constipation
13. Lakini pia kwa wakati mwingine ugonjwa wa Masundosundo au kwa kitaalam Genital warts huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili
VIPIMO VYA TATIZO HILI
Mgonjwa huweza kuchukuliwa history ya tatizo lake lilivyoanza, Kufanyiwa ukaguzi kwa njia mbali mbali kama vile; kuingiza kidole sehemu ya haja kubwa, kutumia kipimo cha Endoscopy n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA
Tiba ya tatizo hili huanza kulingana na sababu za tatizo lenyewe,hivo kama tulivyochambua sababu mbali mbali hapo juu,ndivo na tiba zake huwa mbali mbali, ila kwa ujumla mgonjwa huweza kupata tiba kama vile;
• Matumizi ya baadhi ya dawa za kuondoa kabsa maumivu
• Matumizi ya dawa za kulainisha choo yaani stool softers pamoja na dawa za kulainisha misuli ya sehemu ya haja kubwa
• Kula vyakula na matunda yenye nyuzi nyuzi yaani Fibers kama maembe,machungwa,mapapai,
maparachichi n.k
• Huduma ya upasuaji kwa mgonjwa N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Jinsi ya Kupunguza Au Kuzuia kabsa Maumivu sehemu ya Haja Kubwa
Kuna vitu vya kufanya na Kuzingatia(Do) na kuna vitu vingine hushauriwi kuvifanya kabsa(Don't)
Zingatia mambo Haya(Do);
✓ Hakikisha unakunywa maji mengi kila siku
✓ Kula vyakula vyenye fibre au nyuzi nyuzi za kutosha, ikiwemo mboga za majani na matunda
NB: Maji pamoja na vyakula vya aina hii husaidia kulainisha choo chako na kuzuia tatizo la kupata choo kigumu(Constipation)
✓ Fanya Mazoezi ya mwili mara kwa mara(exercise regularly)
✓ Baada ya Kujisaidia haja kubwa,jisafishe na maji safi, au kama unatumia toilet paper, hakikisha inakuwa laini sio ngumu
✓ Tumia dawa za kutuliza Maumivu ikiwemo paracetamol
✓ Oga na maji ya moto ili kupunguza kuwasha na maumivu n.k
Usifanye kabsa Vitu hivi kama una tatizo hili(Don’t)
× usijikune karibu na sehemu ya haja kubwa
× Ukihisi haja kubwa jisaidie, epuka tabia ya kujibana kwa muda mrefu
× Usitumie nguvu sana wakati wa kujisaidia haja kubwa
× Usitumie sabuni zenye kemikali kali karibu na sehemu ya haja kubwa
× Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi au kutumia pombe pamoja na vinywaji vingine vyenye kiwango kikubwa cha caffeine
× Usibebe au kunyanyua vitu vizito sana
× Usitumie dawa jamii ya ibuprofen kama unavuja damu sehemu ya haja kubwa(anus).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!