Huyu ndiye Mwanaume mzee zaidi duniani aeleza siri yake

Huyu ndiye Mwanaume mzee zaidi duniani aeleza siri yake

Mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani ametangaza kuwa hana "siri ya kipekee" kueleza kuhusu kuishi kwake miaka mingi alipokuwa akisherehekea kutimiza miaka 112.

John Tinniswood, ambaye alizaliwa Liverpool tarehe 26 Agosti 1912, aliiambia Guinness World Records "hakujua kabisa" kwa nini ameishi miaka mingi namna hiyo.

Mwanaume huyo ambaye anaishi katika nyumba ya kutunza wazee huko Southport, alikua mwanamume mzee zaidi duniani mnamo mwezi Aprili wakati Juan Vicente Pérez Mora wa miaka 114 alipofariki dunia.

Alisema alikuwa "mchangamfu sana wakati wa ujana wake" na "alitembea kweli kweli", lakini aliamini "hakuwa tofauti" na mtu mwingine yeyote, akiongeza kuwa: "Kuishi miaka mingi au michache, ni kitu ambacho huna uwezo nacho."

Bw Tinniswood, ambaye alizaliwa mwaka ambapo meli ya Titanic ilizama, alisema anatimiza miaka 112 "akiwa na matumaini ya kipekee".

"Kwa nini nimeishi miaka mingi hivyo, sijui hata kidogo," alisema. "Siwezi kufikiria siri yoyote ya kipekee niliyo nayo.

"Nilikuwa na shughuli nyingi kama kijana, nilitembea sana ... Ikiwa hilo lilikuwa na uhusiano wowote na umri mrefu, sijui.

"Lakini kwangu, sio tofauti. Hakuna cha upekee hata kidogo."

Bw Tinniswood alizaliwa miaka 20 baada ya klabu yake ya kandanda anayoipenda zaidi ya Liverpool kuanzishwa.

Alikuwa na miaka miwili wakati Vita vya Kwanza vya Dunia vinaanza na alikuwa ametoka tu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 27 Vita vya Pili vya Dunia vilipoanza.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!