Ibuprofen inatibu nini? Ibuprofen inatibu magonjwa gani?

 


Ibuprofen inatibu nini? Ibuprofen inatibu magonjwa gani?

Dawa ya Ibuprofen ni miongoni mwa dawa ambazo hutumika mara kwa mara, kwa kiliona hilo,katika makala hii tumechambua baadhi ya matumizi yake pamoja na tahadhari juu ya dawa hii.

Soma zaidi hapa kwenye makala hii..!!!

Ibuprofen inatibu nini?

Dawa ya Ibuprofen ni dawa ambayo ipo kwenye kundi la nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs),

✓ dawa hii hutumika kuondoa maumivu mbali mbali mwilini(pain&tenderness), uvimbe na kukakamaa(stiffness) kunakosababishwa na aina mbali mbali za  ugonjwa wa baridi yabisi ikiwemo;

  • osteoarthritis
  • Pamoja na  rheumatoid arthritis

✓ Dawa ya Ibuprofen pia hutumika kuondoa au kutuliza maumivu yanayotokea mwanamke akiwa kwenye kipindi cha hedhi(menstrual pain).

✓ Dawa ya Ibuprofen huweza kushusha na kupunguza Homa

✓ Dawa ya Ibuprofen huweza kutuliza maumivu ya kichwa,

✓ Dawa ya Ibuprofen huweza kutuliza maumivu ya misuli

✓ Dawa ya Ibuprofen huweza kutuliza maumivu ya Jino

✓ Dawa ya Ibuprofen huweza kutuliza maumivu ya mgongo n.k

Je Dawa ya Ibuprofen hufanya kazi vipi?

Ibuprofen ni dawa kwenye kundi la nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs),

dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia mwili kuzalisha vitu vinavyosababisha;

  • MAUMIVU-pain
  • HOMA-fever
  • pamoja na KUVIMBA-Inflammation.

Tahadhari juu ya Matumizi ya Dawa ya Ibuprofen(IMPORTANT WARNING):

Mbali na dawa ya Aspirin,Watu wanaotumia dawa zote jamii ya nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen, wanaweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la shambulio la moyo(heart attack) au ugonjwa wa kiharusi(stroke) kuliko wale ambao hawatumii dawa kama hizi,

Matukio haya yanaweza kutokea bila taarifa yoyote na yanaweza kusababisha kifo.

Matatizo haya yanaweza kutokea wakati wowote wakati wa matibabu, lakini hatari inaweza kuwa kubwa zaidi kwa watu wanaotumia dawa jamii ya NSAIDs kwa muda mrefu au kwa viwango vya juu zaidi.

Usichukue au kutumia dawa jamii ya NSAIDs kama vile ibuprofen ikiwa kwa hivi karibuni umepata tatizo la mshtuko wa moyo au shambulio la Moyo, isipokuwa kama umeelekezwa na daktari wako.

Article sources checked In:

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!