Je unaweza ukachukua muda gani kubeba mimba baada ya kutoa Vijiti?

 


Je unaweza ukachukua muda gani kubeba mimba baada ya kutoa Vijiti?

Muda gani unaweza kupata mimba baada ya kuacha kutumia njia za uzazi wa mpango?

Hii inaweza kutegemea na aina ya njia uliyotumia, njia inachukua muda gani mpaka kurudi kwa Hedhi, njia inachukua muda gani mpaka kurudi kwenye mzunguko wako wa kawaida wa hedhi, afya yako kwa ujumla, pamoja na hali ya uzazi kwa mpenzi wako(partner’s fertility condition),Umri n.k.

Kwa Mujibu wa "American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG)";

kwa wanandoa wenye umri wa miaka 20 mpaka 30, karibu mwanamke 1 kati ya 4 anaweza kupata mimba wakati wa mzunguko wowote wa hedhi. Lakini hadi Kufikia umri wa miaka 40, nafasi ya kupata mimba inakaribia 1 kati ya 10.

Ni muhimu pia kukumbuka kuwa watu hutofautiana,hivo Jaribu kutovunjika moyo ikiwa mchakato unachukua muda mrefu kwako kuliko vile unavyotarajia.

Uchunguzi mmoja kwenye utafiti wa mwaka 2018 ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 83% ya wanawake wanaoacha kutumia njia za uzazi wa mpango zenye vichocheo ndani yake(hormonal birth control) wanaweza kupata mimba ndani ya miezi 12 ya kwanza.

Je unaweza ukachukua muda gani kubeba mimba baada ya kutoa Vijiti?

Uwezo wa mwanamke kubeba Ujauzito baada ya kuacha kutumia vijiti kama njia ya uzazi wa mpango hurejea ndani ya muda mfupi,Tafiti na machapisho mbali mbali yanathibitisha hilo.

1. Kwa Mujibu wa Healthlines;

Unaweza kupata mimba mapema kwenye wiki baada ya kuondolewa kwa Njiti(implant).

Lakini kama ilivyo kwa njia nyinginezo nyingi za Uzazi wa mpango zenye vichocheo; mwili wako unaweza kuhitaji kurekebisha mzunguko wako wa hedhi, na hii inaweza kuchukua miezi kadhaa.

2. Kwa Mujibu wa WebMd;

Kwa habari ya KiPandikizi/Njiti: Mara moja unaweza kubeba mimba mara tu unapoondoa kipandikizi kama njia ya kuzuia usibebe mimba.

3. Kwa Mujibu wa Shinesa;

Kuna kurudi kwa haraka kwenye uwezo wa kubeba mimba baada ya Kijiti kama njia ya uzazi mpango kuondolewa. Watu wengi hurudi kwenye mzunguko wao wa kawaida wa hedhi na uwezo wa kuzaa ndani ya mwezi mmoja baada ya kuondoa kipandikizi. Ikiwa hutaki kuwa mjamzito unahitaji kutumia njia nyingine ya kuzuia usibebe mimba mara tu kijiti kinapoondolewa.

4. Kwa Mujibu wa Deborah lerner:Chief Medical Officer;

Unapaswa kudhani uwezo wa kubeba mimba utarudi mara moja. Baadhi ya wanawake wamepata mimba ndani ya siku 7-14 baada ya kipandikizi kuondolewa. Ikiwa unajaribu kikamilifu kupata mimba na una umri wa chini ya miaka 35 unaweza kufanikiwa ndani ya mwaka mmoja, wanawake wengi wenye umri huu watapata mimba ndani ya mwaka mmoja. Ikiwa zaidi ya mwaka umepita, ni wakati wa kushauriana na daktari.

Kwa wanawake wenye umri wa miaka 35 na zaidi, wanapendekezwa kumuona daktari ikiwa miezi 6 imepita bila kushika mimba. Katika umri wowote, ikiwa unajaribu kupata Ujauzito, hakikisha unatumia Vitamini supplements ambazo zinajumuisha 400 mcg ya Folic acid ili kusaidia kuzuia kasoro kwa Mtoto wakati anazaliwa(birth defects).

5. Kwa Mujibu wa nhs;

Mara tu kipandikizi kitakapoondolewa, hutakingwa tena dhidi ya ujauzito

"As soon as the implant has been removed, you'll no longer be protected against pregnancy".



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!