Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME(JINSI YA KUONGEZA MANII)



 JINSI YA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME(JINSI YA KUONGEZA MANII)


Hizi hapa ni baadhi ya tips za kuwasaidia wanaume wenye tatizo la Mbegu chache au kwa kitaalam hujulikana kama Low sperm count. Tips hizi zitakusaidia kuongeza mbegu za kiume au manii


1. Kupunguza uzito wa mwili, Watu wengi hawajui kwamba, kama una tatizo la uzito kuwa mkubwa(overweight/obesity) huweza kuathiri mpaka mfumo wako wa uzazi,


Baadhi ya tafiti zinaonyesha mtu mwenye shida ya uzito mkubwa akipunguza uzito wake husaidia sana kuboresha afya ya mbegu za kiume(overall sperm health) ikiwemo kuongeza Semen Volume,concentration pamoja na mobility,


Hivo hakikisha unapunguza uzito wako wa mwili kama una shida hii ya uzito mkubwa(Overweight).


2. Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili, mbali na faida lukuki za mazoezi ikiwemo kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, pia mazoezi husaidia sana kwenye afya ya uzazi ikiwemo swala la mbegu za kiume,


Hivo hakikisha unafanya mazoezi ya mwili angalau kwa dakika 30 au nusu saa kila siku kwa ajili ya afya ya mwili pamoja na afya ya uzazi.


3. Hakikisha unapata Vitamins D,C,E Pamoja na madini ya Calcium vyote hivi ni muhimu kwenye afya ya uzazi,


Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba kwa mwanaume ambaye anapata 1,000mg za Vitamin C kila siku husaidia sana kuongeza sperm concentration pamoja na mobility hivo huongeza uwezo wa mwanaume kutungisha mimba,


Na utafiti huo unazidi kuonyesha kwamba, wanaume ambao hupata kiwango kidogo cha Vitamin D wanakuwa na uwezo mdogo sana wa kutungisha mimba.


4. Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi, Miongoni mwa vitu ambavyo huchangia uwepo wa tatizo la mbegu chache kwa wanaume au Low sperm count ni pamoja na matumizi ya Pombe kupita kiasi


5. Epuka uvutaji wa sigara ikiwemo tumbaku,ugoro, au vilevyi vingine kama vile Coccaine n.k


6. Jikinge ukiwa kwenye mazingira ya kemikali, heavy metals,solvents,Au dawa za kuua wadudu(pesticides) kwani vyote hivi huweza kuathiri sperms.


7. Vaa nguo za ndani ambazo hazibani sana na zenye material ya pamba(cotton boxers) ili kuruhusu hewa kupita na kuepuka joto zaidi,


Kumbuka moja ya vitu muhimu kwenye utengenezaji wa mbegu za kiume ni pamoja na joto(temperature),


Hivo uwepo wa korodani nje ni mahususi kabsa ili kuwa na joto kiasi(moderared temperature) ambalo litasaidia katika utengenezaji wa mbegu za kiume.


8. Pata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala, hakikisha unaondoa Stress au msongo wa mawazo,maana vyote hivi huweza kuathiri mpaka uzalishwaji wa Mbegu za kiume


9. Epuka matumizi ya dawa hovio,Tumia dawa hizi kwa uangalifu na maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya;


- Baadhi ya antibiotics,Anti-Inflammatories,Antipyschotics,Antidepressants,Anabolic steroids,methadone n.k


10. Epuka matumizi ya madawa kama Vumbi la Congo n.k na tumia dawa kama Viagra kwa maelekezo maalumu kutoka kwa wataalam wa afya.


Pia tafiti zinaonyesha Dawa za asili ambazo hujulikana kama ashwagandha au Indian Ginsey,zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu na kusaidia sana wanaume wengi wenye shida hii. Japo faida na hasara za matumizi yake huhitaji utafiti zaidi(Research).


11. Hakikisha unakula vyakula ambazo vitakupa health fat kama vile;Polyunsaturated fats ambayo ni muhimu sana kwa afya ya mbegu za kiume hasa kwenye utengenezaji wa sperm membrane,


aina hii ya Fats ina omega-3 and omega-6.


Epuka matumizi ya chakula ambayo yatakupa unhealthful fat,


Utafiti huu ambao ulifanyika Mwaka 2014 Nchini Spanish kwa wanaume 209 wenye umri wa miaka 18–23 ulionyesha kwamba,

Wanaume hao walikuwa wanatumia kiwango kikubwa cha trans fatty acids na wakati huo huo tatizo la Low sperm count lilionekana kwao.


12. Hakikisha unapata madini ya ZINC pamoja na FOLATE, Bila shaka umekuwa ukisikia sana habari za Zinc kwenye swala la mbegu za kiume, yeah ni kweli Zinc ni muhimu sana kwenye mbegu za kiume ikiwemo faida ya kuongezea mwendo mbegu za kiume yaani mobility.


Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba ukipata Zinc pamoja na Folate kwa kiwango kinachotakiwa mwilini hata afya ya mbegu za kiume(Overall sperm health) ikiwemo concentration pamoja na Count huongezeka sana.


KUMBUKA; Ni salama na Unaweza kutumia supplements ambazo zina virutubisho vinavyotakiwa kama vile Vitamins,Madini(Minerals),antioxidants n.k, ila Mwili hauwezi kufanya ufyonzwaji kwa urahisi zaidi kama mtu ambaye anakula vyakula vyenye virutubisho hivi.


Hivo badala ya kukimbilia Supplements, kula vyakula vyenye virutubisho hivi itasaidia mwili kufanya ufyonzwaji kwa urahisi zaidi na kwa haraka,


"The best way to increase sperm count naturally may be to increase the consumption of foods high in sperm-friendly nutrients, such as vitamin C, antioxidants, and polyunsaturated fats.Than taking Supplements directly".


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments