Ticker

6/recent/ticker-posts

Jinsi Ya Kupima Presha Kwa Usahihi



 JINSI YA KUPIMA PRESHA KWA USAHIHI

Ni kweli kwamba kwa hivi sasa watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la presha au shinikizo la Damu, iwe ni Presha ya kupanda au presha ya kushuka, Na wataalam wa afya wanaendelea kushauri mtu kucheck presha yake mara kwa mara kabla ya matumizi ya dawa za presha.

Swali ni je watu wana elimu ya kutosha kuhusu kujipima presha kwa usahihi? hasa wagonjwa wa Presha? Soma makala hii kuhusu tips mbali mbali au baadhi ya vitu muhimu vya kuzingatia wakati wa upimaji wa Presha ili kupata majibu sahihi.

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA UPIMAJI WA PRESHA

1. Hakikisha mashine au kifaa chako cha kupima presha kinafanya kazi vizuri, kama kinatumia Betri hakikisha betri hazijaisha,na kama ni chaji hakikisha kimechajiwa vizuri,na kama ni mannual hakikisha kila kitu kipo sawa ikiwa ni pamoja na mshale uwe unafanya kazi vizuri,unaweza kusoma namba vizuri kwenye mita,mpira au cuff yenyewe ipo sawa n.k

2. Usipime presha baada ya kunywa vinywaji kama vile Pombe, vinywaji venye Caffeine, Kahawa n.k

3. Usipime presha kama umevuta sigara dakika 30 zilizopita

4. Usipime presha kama ndyo umetoka kufanya mazoezi,kukimbia,kutembea n.k, pumzika kidogo kabla ya kuanza kupima presha

5. Wataalam wa afya hushauri hata kama ulikuwa hufanyi kazi yoyote,unashauriwa kutulia angalau kwa dakika 5-10 kabla ya kuanza kupima presha yako

6. Hakikisha unakaa vizuri kwenye kiti,huku miguu hujaikunja(maarufu kama kukunja Nne),kaa kawaida tu,huku ukinyoosha mkono wako ambao upo upande wa Moyo kwa ajili ya kuanza vipimo

7. Hakikisha miguu yako miwili imegusa chini au imekanyaga chini ya Floor wakati unapima presha

8. Usijifunge cuff ya kupimia presha juu ya shati,hakikisha mkono unakuwa wazi na kipimo kinagusa ngozi ya mwili wako

9. Pia hakikisha unafunga cuff kwenye Msuli wa mkono na sio chini ya kiwiko cha mkono au karibia na viganja vya mkono

10. Hakikisha mpira wa kipimo chako unaangalia kwa juu na sio nyuma ya mkono wako

11. Pia unashauriwa Usiongee wakati wa kupima presha yako

12. Hakikisha unarudia kupima zaidi ya mara moja ili kulinganisha majibu ya kwanza na ya pili,na endapo tofauti ni kubwa sana mfano kwa zaidi ya points 10 rudia kupima kwa mara ya tatu

13. Unashauriwa kuacha kupima presha kwa mazoea,hakikisha unacheck presha yako kila mara unapohisi hali ya tofauti kama vile; kizunguzungu,maumivu makali sana ya kichwa n.k

14. Pia kupima presha kwa mara ya kwanza ukakuta ipo juu haimaanishi tayari wewe ni mgonjwa wa Presha ya kudumu,unaweza kurudia baada ya wiki ukakuta huna hilo tatizo tena,hivo unashauriwa kucheck mara kwa mara,japo endapo baada ya vipimo presha yako ikawa 180/110 mm Hg au zaidi,unashauriwa kuanza tiba mara moja hata kama ndyo siku ya kwanza kupima. N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments