Jinsi ya kusoma Kipimo hiki cha UKIMWI na Kaswende(Syphilis) Kwa Pamoja
Jinsi ya kusoma Kipimo hiki cha UKIMWI na Kaswende(Syphilis) Kwa Pamoja,
Kuna baadhi ya Vipimo kama kwenye Picha hapo hupima maambukizi ya Ukimwi(HIV/AIDS) Pamoja Na Ugonjwa wa Kaswende(syphilis) kwa Pamoja,
Hivo wewe bila Kujua, unaweza kuwa hauna maambukizi ya UKIMWI,ila una Ugonjwa wa KASWENDE(syphilis) halafu Kipimo chako ukashangaa kina mistari miwili,
Sasa kwa vile ulikariri ukiona Mistari miwili tu, tayari unasema una Maambukizi ya UKIMWI, NO..!!
Kuwa makini hapa na vipimo hivi, Soma maelekezo ya Kipimo chako, Mfano wa Kipimo kama hicho ni hapa kwenye Picha ambapo utaona Label kama hivi;
kwa Juu au chini ya kipimo chako lazima uone haya maneno-
HIV/Syphilis
- Halafu C- Control, Ambapo hapa lazima line ichore baada ya kupima bila kujali una tatizo lolote au huna,
Kama kipimo chako hakijachora Mstari wa C-Control Ujue Umekosea Kupima,rudia vipimo vyako
- Syphilis
- HIV
SASA BASI:
(1) Kipimo hiki kikichora Mistari 3 yaani kwenye C,Syphilis na HIV,
Basi una vyote viwili, Maambukizi ya UKIMWI pamoja na Ugonjwa wa KASWENDE
(2) Kipimo kikichora Mistari 2, yaani kwenye C na Syphilis,
Basi una ugonjwa Wa Kaswende
(3) Lakini Kipimo kikichora Mistari 2, yaani kwenye C na HIV,
Basi Ujue una maambukizi ya Ukimwi.
Hayo ndyo maelezo mafupi Juu ya aina Hii ya kipimo;
MAMBO YA KUZINGATIA HAPA
- hakikisha umeangalia Expire Date ya Kipimo chako
- Fahamu Kipimo chako vizuri kinapima Magonjwa gani, Mfano hiki kinapima vitu viwili,Maambukizi ya UKIMWI pamoja na KASWENDE
- Hakikisha baada ya Kusoma Kipimo chako Uone C-CONTROL LINE IMECHORA, Kama Control Line Haijasoma Umekosea Kupima, Rudia kupima.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!