kidonda cha upasuaji kuchelewa kupona,chanzo chake
Baada ya kufanyiwa upasuaji kidonda kinaweza kuchelewa kupona na kuanza kuwa na Usaha wa Mara kwa Mara n.k
Je chanzo cha hali kama hii ni nini? endelea kufwatilia makala hii itakusaidia kujua
DALILI AMBAZO HUWEZA KUJITOKEZA NI PAMOJA NA;
- Kuanza kupata maumivu makali ya gafla kwenye kidonda ambayo hayakuepo
- Kidonda kuanza kuvuja damu
- Joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na Homa
- Kidonda kuanza kutoa usaha mara kwa mara
- Sehemu ya kidonda kuanza kuvimba n.k
CHANZO CHA KIDONDA CHA UPASUAJI KUCHELEWA KUPONA,
- Kidonda kufunguka chenyewe(wound reopen), kidonda cha upasuaji kinaweza kisipone haraka kwasababu kimeachia nyuzi,kufumuka au kuburst hali ambayo hupelekea uhitaji wa kukiangalia tena na ikiwezekana kushonwa upya.
- Maambukizi(infections), Baada ya kidonda kushambuliwa na vimelea vya magonjwa kama vile bacteria n.k huweza kuchelewa kupona, Tatizo hili huchangia kwa asilimia kubwa vidonda kuchelewa kupona na wakati mwingine kuharibika kabsa.
- Tatizo la Unene kupita kiasi(Obesity), Unene huweza kuchelewesha au kupunguza kasi ya kidonda kupona kwa sababu ya kuwa na mtiririko mdogo wa damu pamoja na ugavi wa hewa ya Oxygen kwenye seli za mafuta ikilinganishwa na tishu nyingine.
-Utapiamlo(Malnutrition),Utapiamlo huweza pia kupunguza kasi ya kidonda kupona kwa sababu ya ukosefu wa vitamini, protini na virutubisho vingine vinavyohitajika ili kidonda kupona.
Hypoalbuminemia, ukosefu wa protein albumin, huhusishwa pia na kuchangia sana tatizo la vidonda kufunguka au kwa kitaalam hujulikana kama dehiscence.
- Uvutaji wa sigara, kuvuta sigara hupunguza ugavi wa oksijeni kwenye tishu(oxygenation) ambayo ni muhimu kwa uponyaji wa haraka.
- Matatizo ya mishipa yaani Peripheral vascular, respiratory, pamoja na cardiovascular disorders, Haya yote huathiri ugavi wa oksijeni, kama ilivyo kwa mtu mwenye shida ya upungufu wa damu yaani anemia, kisukari na shinikizo la damu.
- Saratani. Upasuaji wa kutibu tatizo la saratani kama vile saratani ya kichwa na shingo au saratani ya utumbo mpana huweza kupelekea kidonda kufunguka na kuchelewa kupona,
- Umri. Watu wazima zaidi ya umri wa miaka 65 wana uwezekano mkubwa wa kuwa na hali zingine ambazo hupunguza mchakato wa uponyaji wa kidonda.
- Steroids, Matumizi ya dawa za steroid hupunguza kasi ya uponyaji wa Kidonda.
- Uzoefu wa upasuaji. Ikiwa daktari wako wa upasuaji hana uzoefu, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi wakati wa upasuaji, au kidonda kutokushonwa vizuri,Hii inaweza kusababisha kidonda kufunguka tena. N.k
MAMA ULIYEJIFUNGUA KWA UPASUAJI FANYA HAYA ILI KUPONA HARAKA
Haya ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu sana kwa mama ambaye kajifungua kwa njia ya Operation(upasuaji), na yatamsaidia mama huyu kupona haraka.
- Hakikisha unajitahidi kufanya mazoezi mbali mbali kama vile; kutembea n.k.
Moja ya faida kubwa ya mazoezi kwa mama mwenye kidonda cha upasuaji au Operation ni kusaidia kurudusha mzunguko wa damu kwenye mishipa ya damu eneo la kidonda hivo kufanya seli kuwa na uhai na kidonda kupona kwa haraka zaidi
- Usafi wa mwili ni muhimu sana ikiwa ni pamoja na eneo la kidonda, baadhi ya wakina mama baada ya kufanyiwa upasuaji hawaogi tena mpaka wapone, hali ambayo huwa hatari kwa kidonda na kuweza kusababisha kidonda kushambuliwa na wadudu kama Bacteria, kidonda kuoza n.k
- Zingatia lishe bora hasa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha proteins husaidia kurepair na kuponyesha haraka sana vidonda
- N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!