Ticker

6/recent/ticker-posts

KIDONDA UKENI AU MALENGELENGE UKENI,CHANZO NA TIBA



 KIDONDA UKENI AU MALENGELENGE UKENI,CHANZO NA TIBA.

Baadhi ya wanawake hupatwa na tatizo la Kidonda kwenye shavu la uke au kuwa na malenge lenge kwenye mashavu ya Uke,

Je na tatizo hili hutokana na nini? na dalili zake ni zipi?

CHANZO CHA TATIZO HILI

1. Magonjwa ya Zinaa, Kwa asilimia kubwa magonjwa ya zinaa huchangia mwanamke kuwa na vidonda au malenge lenge ukeni,

magonjwa ya zinaa ni mengi,ila baadhi ni kama vile kisonono,kaswende,chlamydia,HIV n.k

2. Mashambulizi ya Fangasi sehemu za Siri,

Pia fangasi hasa jamii ya Candida Albicans huweza kushambulia sehemu za siri za mwanamke na kusababisha;

vidonda,michubuko,miwasho,ngozi ya nje ya uke au kwenye mashavu ya uke kuwa nyekundu zaidi n.k

3. Mashambulizi ya Bacteria, Hapa nazungumzia Bacteria kama vile Streptococcus au mashambulizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke,

ambapo huweza kuambatana na damu wakati wa tendo la ndoa,maumivu makali wakati wa tendo,maumivu chini ya kitovu,uchaufu mweupe au njano kutoka ukeni,vidonda n.k

4. Tatizo la mzio au allergic reaction kutokana na baadhi ya vitu kama vile;

Mwanamke kuwa na allergy kwenye baadhi ya dawa,sabuni za kuogea,mafuta,baadhi ya PEDI,Nguo za ndani n.k

ambavyo vitu hivi huweza kumuunguza kwenye ngozi yake ya ukeni na kumsababishia vidonda

5. Tatizo la kansa au Saratani kwenye eneo la sehemu Za siri n.k

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

- Mwanamke kupata homa au joto la mwili kuwa juu sana kuliko kawaida

- Kuanza kupata mitoki

- Maumivu makali wakati wa kukojoa,kutembea au kuchuchumaa

- Kutokwa na maji maji au damu ambayo huonekana kwenye nguo za ndani

- Miwasho sehemu za siri,ngozi kubadilika rangi na kuwa nyekundu zaidi,vipele kama vijipu hatimaye baadae hugeuka kuwa vidonda au malengelenge.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments