KITOVU CHA MTOTO KUTOA MAJI,CHANZO NA TIBA

 KITOVU CHA MTOTO KUTOA MAJI,CHANZO NA TIBA

Baada ya mtoto kuzaliwa, mtoa huduma hukata kitovu cha mtoto yaani umbilical cord kisha kuacha kipande kidogo sana ambacho hukauka na kudondoka chenyewe ndani ya wiki moja na kuendelea baada ya mtoto kuzaliwa.

Wakati mwingine ile sehemu ya kitovu cha mtoto huweza kushambuliwa na vimelea vya magonjwa kama vile bacteria,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama omphalitis.

Tatizo hili halitokei sana kwenye nchi zilizoendelea ambapo inakadiriwa kwamba ni asilimia 0.7% tu kwa mataifa yaliyoendelea(developed nations).

Endapo maambukizi haya ya Bacteria kwenye kitovu cha mtoto hayajapata tiba,huweza kusambaa zaidi ya hapo,na hata kusababisha vifo,ambapo inakadiriwa kuwa ni kwa asilimia  7–15% ya vifo(mortality rate).

HIZI HAPA CHINI NI BAADHI YA DALILI ZA MAAMBUKIZI KWENYE KITOVU CHA MTOTO BAADA YA KUZALIWA

- Kitovu cha mtoto kutoa Maji maji

- Kitovu cha mtoto kutoa usaha

- Kitovu cha mtoto kuvuja damu kupita kawaida

- Kitovu cha mtoto kuwa na harufu mbaya

- Ngozi ya eneo la kuzunguka kitovu kuwa nyekundu zaidi

- Kuwa na vipele eneo la kuzunguka kitovu cha mtoto

- Mtoto kuwa na homa au joto la mwili kuwa juu sana

- Mtoto kukataa kunyonya kabsa au kushindwa kunyonya

- Mtoto kulala kupita kawaida

- Mtoto kutokulala kabsa

- Mtoto kulia sana mara kwa mara

- Mtoto kuishiwa nguvu kabsa na kulegea sana n.k

BAADHI YA SABABU ZINAZOONGEZA UWEZEKANO WA KITOVU CHA MTOTO KUSHAMBULIWA NA VIMELEA VYA MAGONJWA KAMA BACTERIA

• Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo zaidi kuliko kawaida(low birth weight)

• Mama mjamzito kuwa na matatizo kama vile chorioamnionitis au maambukizi mengine wakati wa kujifungua

• Chupa ya uzazi kupasuka na mama mjamzito kukaa kwa masaa 24 au zaidi ya masaa 24 kabla ya kujifungua

• Mtoa huduma kutumia vifaa vichafu( unsterile and unclean instruments) wakati wa kukata kitovu cha mtoto

• Mtoto kuzaliwa kwenye mazingira ambayo sio salama kama vile nyumbani n.k

• Wazazi au walezi kutokitunza vizuri kitovu baada ya mtoto kuzaliwa,na wengine kuwa na Imani potofu za kupaka vitu mbali mbali kwenye kitovu cha mtoto kama vile Mavi ya ng'ombe eti ili kitovu cha mtoto kidondoke mapema na kupona haraka n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!