KUCHUTAMA/KUCHUCHUMAA(SQUATTING TOILETS):NJIA SALAMA YA KWENDA HAJA KUBWA

 KUCHUTAMA/KUCHUCHUMAA(SQUATTING TOILETS):NJIA SALAMA YA KWENDA HAJA KUBWA

Kabla ya kuanza kuelezea baadhi ya tafiti mbali mbali ambazo zimefanyika kuhusu faida za kujisaidia ukiwa umechuchumaa yaani Squatting position, nitoe ufafanuzi kuhusu aina za vyoo,

Kuna vile vyoo vya kukaa kabsa ambavyo mara nyingi hutumika hospitalini kwa ajili ya wagonjwa ambao hawawezi kujisaidia wakiwa wamechuchumaa, ila kwa hapa tunazungumzia squatting toilets kama hapo kwenye picha,

Aina hii ya vyoo itakulazimu ujisaidie haja kubwa ukiwa umechuchumaa yaani squatting position, na wataalam wa afya husema kujisaidia kwa staili hii kuna faida zaidi kuliko kujisaidia ukiwa umekaa kabsa(vyoo vya kukaa).

FAIDA ZA KUJISAIDIA HAJA KUBWA UKIWA UMECHUCHUMAA(SQUATTING) KULIKO UKIWA UMEKAA KABSA NI PAMOJA NA;

- Kusaidia haja kubwa itoke haraka,kwa urahisi zaidi, na ujisaidie kinyesi chote mpaka kiishe, hali hii husaidia kuzuia tatizo la kinyesi kukwama wakati wa kujisaidia, na kukuepusha na matatizo mengine mbali mbali kama vile; kuvimba kwa njia ya haja kubwa,michubuko,kuvimba kwa kidole tumbo(appendicitis) n.k

- Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia pia katika kulinda Nerves za tezi dume(prostate),kibofu cha mkojo, pamoja na tumbo la uzazi yaani uterus ambavyo huweza kuharibiwa kabsa

- Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia kulinda valve yaani Ileocecal valve, kati ya utumbo mkubwa na utumbo mdogo, tofauti na mtu ambaye hujisaidia akiwa amekaa, valve hizi hukosa kabsa support na mara nyingi huweza kutengeneza uwazi au Kuleaks hali ambayo huweza kupelekea uchafu kuingia kwenye utumbo mdogo

- Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia kurelax misuli mbali mbali kama vile Puborectalis muscle na kusaidia mtu kujisaidia  kwa urahisi zaidi

- Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia kusupport utumbo mkubwa yaani colon na kukukinga na matatizo mbali mbali kama vile; hernia,Diverticulosis,Pelvic organ prolapse n.k

- Kutokana na tafiti mbali mbali za afya, Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia kupunguza tatizo la bawasiri au hemorrhoids kama ilivyoripotiwa na "Clinical health Research"

- Kwa Mama Mjamzito, Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia kuepuka mgandamizo mkubwa wa Uterus na pia huweza kuwa ni mojawapo ya mazoezi ambayo huweza kumsaidia mama mjamzito kujifungua kwa urahisi zaidi

- Kujisaidia haja kubwa kwa staili hii husaidia hata mkojo kutoka vizuri na kusaidia misuli ya kwenye kibofu cha mkojo kufanya kazi vizuri zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!