KUTOKA VIPELE KWENYE ULIMI,CHANZO CHAKE
Baadhi ya watu hupata shida hii ya kutokwa na vipele au vidonda kwenye ulimi hali ambayo huweza kuwasababishia maumivu hasa wakati wa kula.
Hizi hapa chini ni baadhi ya Sababu za tatizo hili;
- Kuumia, ulimi huweza kupata jeraha, kidonda au vipele kama vijipu baada ya kupata mchubuko ambayo hutokana na sababu mbali mbali kama vile kujing'ata, kula vitu vya moto sana,kuungua n.k
- Uwepo wa Magonjwa kwenye kinywa ikiwemo Maambukizi ya fangasi(Oral thrush/yeast infection),
- Shida ya kuvimba kwenye ulimi ambayo hujulikana kwa kitaalam kama enlarged papillae
- Maambukizi ya virusi kama vile Human Papilloma Virus(HPV) n.k
- Ugonjwa wa kaswende au syphilis
- Mtu kuwa na allergies au mzio kwenye vitu mbali mbali kama vile baadhi ya dawa za kunywa, vyakula n.k
- Uvutaji wa Sigara, ambao huweza kuleta madhara mbali mbali ikiwemo; kuvimba kwa ulimi,ulimi kuwa na vipele au vidonda, harufu mbaya mdomoni, meno kuharibika, cancer ya kinywa n.k
- Upungufu wa Vitamins kama vile vitamins B12, Madini ya chuma(Iron), au Folate
na wakati mwingine mabadiliko ya vichocheo(hormones) mbali mbali mwilini
- Tatizo la Neuralgia,ambalo huhusisha kuharibika kwa nerves
- Tatizo la Lichen planus, ambalo huhisisha ngozi laini(chronic skin issues)
- Ugonjwa wa Behcets ambao huhusisha mishipa ya damu kuvimba kwenye maeneo mbali mbali mwilini
- Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile dawa jamii ya Naproxen(Aleve) n.k
- Tatizo la Kansa ya kinywa yaani Oral cancer n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!