KUTOKWA NA MAJI MAJI SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAUME
Penile discharge- Hili ni Tatizo la kutokwa na maji maji au usaha kwenye uume, Wanaume wengi hupatwa na tatizo hili la kutokwa na maji maji sehemu za siri na kwa baadhi ya hao hutokwa na usaha sehemu za siri au kwenye uume, tatizo hili huweza kutokana na sababu zaidi ya moja japo kwa asilimia kubwa ya wanaume hupatwa na tatizo hili kutokana na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya Zinaa.
Kutokwa na maji maji au usaha kwenye uume huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile; kupata maumivu wakati wa kukojoa au mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo, rangi ya uume kubadilika na kuwa nyekundu zaidi, kupatwa na miwasho sehemu za siri ikiwa ni pamoja na kwenye korodani au katikati ya njia ya haja kubwa na korodani n.k.
SABABU ZA KUTOKWA NA MAJI MAJI SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAUME
1. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa, kwa asilimia kubwa wanaume hupatwa na tatizo la kutokwa na maji maji au usaha kwenye uume kutokana na mashambulizi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa kama vile;
• Ugonjwa wa kisonono au Gonorrhea
• Tatizo la Chlamydia
• Tatizo la Trichomonas
• Na kwa asilimia ndogo sana maambukizi ya Genital herpes huweza kuchangia mwanaume kupatwa na tatizo la kutokwa na maji maji kwenye uume
2. Maambukizi ya bacteria kwenye mfumo wa njia ya mkojo au Urinary tract infection(UTI)
3. Sababu zingine ni pamoja na;
- Maambukizi yaani Mycoplasma genitalium infection
- Ureaplasma urealyticum infection
- Kuvimba kwa njia ya mkojo au tatizo la Urethritis
- Mwanaume Kupata tatizo la Saratani ya uume n.k
MATIBABU YA TATIZO LA KUTOKWA NA MAJI MAJI SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAUME
Tatizo hili hutibika kutokana na chanzo chake,hivo mgonjwa atapata tiba kulingana na chanzo husika, ila kwa ujumla wake zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kutibu tatizo hili, Na
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!