kuwashwa sehemu ya haja kubwa,chanzo na Tiba yake
Tatizo la kuwashwa sehemu ya haja kubwa huweza kuambatana na;
• Mtu kuhisi hali ya kuungua
• Kubadilika rangi ya ngozi na kuwa nyekundu eneo hili la haja kubwa
• Uwepo wa michubuko au vidonda
• Kuvimba Sehemu ya haja kubwa
• Kutokea Vipele au Rashes sehemu ya haja kubwa n.k
ONANA NA DAKTARI AU WATAALAM WA AFYA KAMA;
- Miwasho sehemu ya haja kubwa ni mikali sana na haiishi au niendelevu
- Unajisaidia choo kimechanganyika na damu
- Unatokwa na haja kubwa bila kujizuia
- Unakosa usingizi kwa sababu ya miwasho
- Umepatwa na vipele,michubuko au vidonda ambavyo haviponi n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUWASHWA SANA SEHEMU YA HAJA KUBWA
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu ambazo huweza kuchangia uwepo wa Tatizo hili;
1. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo; Magonjwa ya Zinaa, Tatizo la Minyoo(pinworms), au Maambukizi ya Fangasi
2. Uwepo wa magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile; psoriasis,contact dermatitis au atopic dermatitis/eczema(Ukurutu/Pumu ya Ngozi) n.k
3. Msuguano mkali sehemu ya haja kubwa kutokana na kutumia vitu ambavyo hukwaruza wakati wa kujisafisha baada ya haja kubwa, mfano; kutumia karatasi ngumu,magunzi n.k
4. Tatizo la kutokwa na kinyesi bila kujizuia au tatizo la kuharisha kwa muda mrefu, hivi huweza kuchangia pia ngozi ya sehemu ya haja kubwa kuwasha
5. Swala zima la usafi pamoja na utunzaji wa ngozi ikiwemo; matumizi ya products zenye kemikali kali kama baadhi ya Sabuni wakati wa kujisafisha,
Kutumia Toilet paper au nguo za ndani zenye chembe chembe kali zilizowekwa kwenye manukato au rangi zilizotumika kutengenezea vitu hivo.
kujisafisha kwa fujo sana(washing too aggressively) n.k, vyote hivi huweza kuwa chanzo cha wewe kuanza kuwashwa sehemu ya haja kubwa
6. Sababu zingine ni pamoja na; tatizo la bawasiri au hemorrhoids, Uvimbe sehemu ya haja kubwa(anal tumors) N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!