Ticker

6/recent/ticker-posts

kuwashwa ukeni kabla ya hedhi,chanzo chake na Tiba



Kuwashwa ukeni kabla ya hedhi au Period,chanzo chake na Tiba

Mwanamke anaweza kupatwa na tatizo hili la kuwashwa Ukeni kabla ya hedhi kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo;

  • Mabadiliko ya vichocheo ambayo hutokea kipindi hiki,
  • maambukizi ya magonjwa n.k

Katika Makala hii tutachambua Zaidi kuhusu kuwashwa ukeni kabla ya hedhi,chanzo chake na Tiba yake.

CHANZO CHA KUWASHWA UKENI KABLA YA HEDHI

Zipo sababu mbali mbali zinazopelekea tatizo la Mwanamke kuwashwa ukeni kabla ya hedhi, na Sababu hizo ni Pamoja na;

- Tatizo la ukavu ukeni yaani Vaginal dryness

Kiwango cha Vichocheo aina ya Estrogen huongezeka sana kipindi cha ovulation,kisha hushuka kwa haraka sana kwenye siku karibia na Hedhi,

Hii huweza kusababisha ukavu ukeni Hali hii ya Vaginal dryness huweza kusababisha uke kuwa na maumivu na kuwashwa hasa wakati wa kufanya mapenzi au kuwashwa ukeni kabla ya hedhi.

Pia hali hii ya ukavu ukeni huweza kutokea kwa Mwanamke anayekaribia ukomo wa hedhi(menopause), na kwa baadhi ya wanawake ambao wametoka kujifungua muda mfupi, au ambao wananyonyesha.

- Kuvimba yaani inflammation

Kuna ushahidi unaonyesha kuwa hedhi huongeza unyeti wa ngozi(skin sensitivity),

Utafiti wa mwaka wa 1991 uligundua kuwa wanawake katika siku ya kwanza ya mzunguko wao wa hedhi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupata mwasho wa ngozi kuliko ilivyokuwa siku za baadaye katika mzunguko wao,

Na hii ilitokana na kuvimba kwenye ngozi,hali ambayo hupelekea pia  kuwashwa ukeni kabla ya hedhi.

- Period products, hapa tunazungumzia vitu ambavyo unavyovitumia ukiwa karibu na hedhi au ukiwa kwenye hedhi kama vile nguo za ndani, pedi au taulo za kike n.k

Vitu hivi pia huweza kuchangia uwepo wa tatizo la kuwashwa ukeni kabla ya hedhi.

Matumizi ya baadhi ya Visodo(Tampons) huweza kufyoza vilainishi asilia ukeni(natural vaginal lubrication) na kusababisha hali ya Ukavu ukeni kisha kuongeza hatari ya kupata tatizo la kuwashwa ukeni kabla ya hedhi,

Hivo hivo kwa baadhi ya nguo za ndani,matumizi ya baadhi ya sabuni n.k huweza kusababisha hali hii ya kuwashwa ukeni kabla ya hedhi,

na wakati mwingine kuleta allergic reaction ya ngozi kwa baadhi ya Wanawake,kisha kupelekea miwasho ukeni.

- Maambukizi ya magonjwa kama vile Fangasi sehemu za Siri(Yeast infection),

Hii pia huweza kupelekea Mwanamke kupata tatizo la kuwashwa ukeni kabla ya hedhi.

- Tatizo la Cyclic vulvovaginitis, ambalo huhusisha maambukizi ya muda mrefu ambayo hutokea tena kabla au wakati wa kipindi cha Hedhi.

Mwanamke mwenye tatizo la Cyclic vulvovaginitis huweza kupatwa na dalili kama hizi;

  • Kuhisi hali ya kuungua ukeni,kuuma,
  • kupatwa na miwasho ukeni au kuhisi hali ya kuchomwa chomwa kabla ya kuanza hedhi
  • Au kuwashwa ukeni kabla ya hedhi

- Tatizo la Bacterial Vaginosis, ambapo huhusisha maambukizi ya bacteria Ukeni,

Haya ni maambukizi ambayo hutokea sana kwa Wanawake wenye umri kuanzia miaka 15-44,

Wanawake wenye tatizo hili hupatwa na hali ya kutoa harufu kama shombo la samaki ukeni(strong fishy odor), hasa baada ya kufanya mapenzi,

Lakini pia huweza kupata dalili zingine kama vile;

  • kutokwa na uchafu mwembamba wenye rangi nyeupe au Kijivu,
  • kupata maumivu wakati wa tendo,
  • kuhisi hali ya kuungua
  • pamoja na kuwashwa ukeni.

- Magonjwa ya Zinaa(Sexually transmitted infections) kama vile kisonono(gonorrhea) huweza kusababisha pia hali hii ya kuwashwa ukeni,pamoja na kutokwa na uchafu wenye harufu.

Maambukizi haya huwa hayazidi kuwa mabaya kabla au wakati wa kipindi cha hedhi. Walakini, watu wengine wanaweza kugundua dalili kwa mara ya kwanza kabla ya kipindi cha hedhi kuanza.

MATIBABU YA TATIZO HILI La kuwashwa ukeni kabla ya hedhi

Kama nilivyokwisha kueleza baadhi ya Sababu za tatizo hili la kuwashwa Ukeni kabla ya hedhi, hata Matibabu yake yatategemea chanzo husika cha tatizo hili, hivo hakuna Tiba moja maalumu(specific treatment) kwa tatizo hili.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, kuwashwa ukeni kabla ya hedhi husababishwa na nini?

Zipo sababu mbali mbali zinazopelekea tatizo la Mwanamke kuwashwa ukeni kabla ya hedhi, na Sababu hizo ni Pamoja na;

Tatizo la ukavu ukeni yaani Vaginal dryness,Kuvimba yaani inflammation,Maambukizi ya magonjwa kama vile Fangasi sehemu za Siri(Yeast infection) n.k

Hitimisho

Tatizo la kuwashwa ukeni kabla ya hedhi ni tatizo ambalo huweza kumpata mwanamke yoyote,

Na Zipo sababu mbali mbali zinazopelekea tatizo la Mwanamke kuwashwa ukeni kabla ya hedhi, na Sababu hizo ni Pamoja na;

Tatizo la ukavu ukeni yaani Vaginal dryness,Kuvimba yaani inflammation,Maambukizi ya magonjwa kama vile Fangasi sehemu za Siri(Yeast infection) n.k

Kama una tatizo hili la kuwashwa ukeni kabla ya hedhi,hakikisha unaongea na wataalam wa afya ili kupata Msaada Zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments