Kwanini Asali hutumika kwenye Vidonda? Faida zake ni zipi?
Watu wametumia asali kwa miaka mingi kusaidia Kuponya majeraha au vidonda, Ingawa sasa tuna njia nyingine nzuri za kuponya majeraha, asali bado inaweza kuwa nzuri kwa kuponya majeraha fulani.
Asali ina asili ya kuzuia bacteria(antibacterial properties) na usawa wa kipekee wa pH ambao husaidia kukuza kiwango cha oksijeni na kusaidia katika uponyaji wa jeraha au kidonda.
Asali ina asili ya anti-oxidant, anti-bacterial na anti-inflammatory, ndyo maana inaweza kutumika kwenye kidonda ili kusaidia uponyaji wa haraka,
Hivo basi,Matokeo haya yanatokana na hatua ya asali kuweza kupambana na bakteria, pili asidi yake ya juu, athari ya osmotic, kuwa na anti-oxidant content pamoja na hydrogen peroxide content.
TAHADHARI; Ni vizuri kutumia asali baada ya uchunguzi wa kina wa kidonda chako pamoja na kupewa maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya. Na ndipo wakiona inafaaa kutumia asali kwa kidonda chako basi unaweza kupata faida za matumizi haya ya asali.
Hakikisha unapaka asali kwenye kidonda safi baada ya kusafishwa,sio unapaka juu ya uchafu
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!