Ticker

6/recent/ticker-posts

kwanini mbu hawezi kuambukiza Ukimwi



kwanini mbu hawezi kuambukiza Ukimwi

Mbu wanaweza kueneza magonjwa mbalimbali, kama vile malaria na homa ya dengue, lakini hawana uwezo wa kusambaza VVU. Hii ni kwa sababu: Hawana T-seli za binadamu zinazohitajika mwilini ili virusi vijizalishe na kuendelea kuishi, Hii inamaanisha kwamba mbu hawawezi kuambukizwa VVU.

T cells ni nini?

T-cells; ni sehemu ya mfumo wa kinga ya mwili yaani body Immunity system na hukua kutoka kwa seli shina kwenye uboho. Hizi zinasaidia kulinda mwili kutokana na maambukizi na zinaweza kusaidia kupambana na saratani. Pia huitwa T lymphocyte na thymocyte.

Kwa Kawaida,Virusi vya Ukimwi(VVU) hushika kwenye vipokezi au receptors kwenye uso wa seli za kinga. Ndipo vinaweza kuathiri seli hizo, kunakili, na kuenea.

Mbu (na wadudu wengine) hawana kipokezi ambacho VVU hutumia kutambua seli za kinga. Hii ina maana kwamba mbu hawawezi kupata maambukizi ya VVU. Badala yake,virusi huvunjwa tu na kumeng’enywa kwenye tumbo la mbu.

Kwa sababu hawawezi kupata maambukizi ya VVU, mbu hawawezi kusambaza VVU kwa binadamu.



Post a Comment

0 Comments