Connect with us

Uzazi/Ujauzito

LINI MAMA MJAMZITO(MAMA KIJACHO) AANZE KLINIKI?

Doctor Ombeni

Published

on

147 Views
0 Comments

LINI MAMA MJAMZITO(MAMA KIJACHO) AANZE KLINIKI?

KABLA hata mwanamke HAJABEMBA MIMBA,kama ana plan ya Kubeba MIMBA,Inashauriwa mwanamke na Mwenzi wake Wafike hospitali kwa ajili ya USHAURI na baadhi ya Uchunguzi, hivo ndyo kiafya Zaidi inashauriwa.

lakini pia mama huyu mara moja anaanzishiwa madini kwajili ya maandalizi ya mtoto, hapa ndipo matumizi ya Fefol au FOLIC ACID huanza ili kuzuia mtoto asije zaliwa na Matatizo kama vile;

  • Tatizo la mgongo wazi,
  • kichwa kikubwa n.k,
  • Lakini pia Vidonge hivi husaidia damu ya Mama Kuongezeka Zaidi

lakini pia kwa wenye magonjwa kama Ukimwi,presha,Homa ya ini yaani Hepatitis unaangaliwa, mfano kama Viral load Ipo chini sio risk kwa kumuambukiza mtoto na mengineyo kama ushauri wa kijumla juu ya lifestyle.

LINI MAMA MJAMZITO(MAMA KIJACHO) AANZE KLINIKI?

Ingawa Protocol za Hospital na hospital huweza kutofautiana kwa habari ya Muda wa kuanza hudhurio la Kwanza la Kliniki kwa Ujauzito; ila Kwa ujumla,MAMA MJAMZITO Anashauriwa AANZE CLINIC MARA TU ANAVYOGUNDUA AMEPATA UJAUZITO au Aanze Hudhurio la kwanza la Ujauzito kabla ya kufikisha wiki 16 za ujauzito.

Mahudhurio ya Kliniki yamegawanyika katika makundi manne kulingana na Umri wa Ujauzito japo yanaweza kuzidi manne kulingana na Hali ya Ujauzito.

  1. Hudhurio la kwanza  ni Ujauzito kabla ya kufika wiki 16
  2. Hudhurio la Pili ni Ujauzito ukiwa na umri wa wiki 20-24
  3. Hudhurio la Tatu ni Ujauzito ukiwa na umri wa wiki 28-32
  4. Na hudhurio la Nne ni Ujauzito ukiwa na umri wa wiki 36-40

Nb; Mahudhurio haya yanaweza kuzidi manne kulingana na Hali ya Ujauzito,mfano mama akiwa na magonjwa mengine kama presha n.k

NB: Ikiwa umegundua una MIMBA,Plan kuanza clinic mapema, Na unatakiwa kwenda na mwenzi wako hasa kwa ajili ya kupata Ushauri pamoja,Kufanya vipimo kama vile vya Ukimwi,Homa ya Ini(hepatitis),group za damu kama Hazipo tofauti.n.k

Mfano: Unakuta mwanamke HANA MAAMBUKIZI ya VVU,mwanaume ANAYO(Discordant couple),Tukipima na kujua hili,Mnazingatia ushauri ili Kumlinda mtoto (ndio FAIDA za kuja mapema).

lakin Pia kama WOTE wanamaambukizi Pia kuna ushauri Tunatoa,Lengo ni kumlinda mtoto asizaliwe na MAAMBUKIZI. kuna FAIDA nyingi sana za kuja kapata Uchunguzi mapema mkiwa wote Wawili.

UMUHIMU WA MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO

Kwa Ujumla wake safari ya kupata Mtoto huanza pale tu mwanamke anapokuwa Mjamzito mpaka atakapofikisha mda wa Kujifungua. Ambapo inaweza kuwa kutoka wiki 0-42 za Ujauzito.

VITU VYA MUHIMU KATIKA MAHUDHURIO YOTE KWA UJUMLA WAKE

➖ Kupata Elimu ya kutosha katika maswala mbali mbali ya afya kama vile; lishe,Usafi,Maandalizi ya Kujifungua,Dalili zahatari kipindi cha Ujauzito na mara tu baada ya kujifungua.
➖ Upimaji wa magonjwa kama Shinikizo la damu,Sukari,protein kwenye Mkojo,Malaria,Uti,Kaswende,Ukimwi n.k
➖ Vipimo juu ya Group la damu la mama na wingi wake wa Damu
➖ Utoaji wa dawa za Kuzuia malaria maarufu kama SP,Dawa za minyoo maarufu kama Mebendazole,na vidonge vyekundu kwa ajili ya kuongeza damu,kuzuia watoto kuzaliwa na matatizo kama mgongo wazi na Vichwa vikubwa.
➖ Kuendelea kuchunguzwa maendelo ya mtoto tumboni ikiwemo,kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto,mlalo wake n.k
➖ Tarehe za matarijio ya kujifungua kujulikana pamoja na maandalizi kamili ya kujifungua
➖ Kuendelea kupata Elimu juu ya Njia sahihi za Kupanga Uzazi
➖ Uchomaji wa Chanjo zote muhimu kwa mama Mfano chanjo muhim ya kuzuia Ugonjwa wa PEPOPUNDA maarufu kama TETENUS

UMUHIMU WA MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO

(1) Mama atapewa Elimu juu ya maandalizi ya kujifungua yaani INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS (IBP),Lishe wakati wa Ujauzito,Usafi wa mwili,Kujua dalili za Hatari kwa Mjamzito,n.k
MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA
Mama kujua vitu vya kuandaa mfano Pesa ya kutosha,Usafiri wa kwenda hosptal,Mtu atakayebaki na Familia pindi mama akiwa hospital, Kuweka vitu vyako pamoja kama kadi la Kliniki,nguo n.k, Kuwa na mtu atakayekupeleka hospital,Kuandaa vifaa kama gloves,makintosh,Chupi,pamba n.k  kama vitahitajika
BAADHI YA DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO
  • kutokwa na Damu ukiwa Mjamzito
  • Kutokwa na uchafu wenye harufu kali ukeni hii ni dalili ya maambukizi kama Fangasi
  • Miguu kuvimba kupita kiasi,mikono pamoja na Uso
  • kuona Maruerue wakati wa Ujauzito
  • kutokumsikia mtoto anacheza tumboni zaidi ya masaa 24 kwa mama ambaye umri wa mtoto kucheza tumboni umefika mfano kuanzia wiki 20-24. endelea kutufwatilia kujua zaidi…
  • Presha kupanda na kuwa na Protein kwenye mkojo,hiki ni kiashiria kikubwa cha Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba
(2) Mama mjamzito atapimwa magonjwa mbali mbali kama Ukimwi,UTI,Fangasi,PID,Kaswende,Malaria,Wingi wa Damu,Group lake la Damu, Presha, na Magonjwa mengine ya zinaa
(3) Mama mjamzito atasaidiwa Kujua Tarehe yake ya Matarijio kwa ajili ya kujifungua ili awe tayari.
(4) Mama mjamzito atachomwa chanjo ya kuzuia Tetenus kama hakuchoma
(5) Mama mjamzito atapewa dawa muhim sana kipindi cha Ujauzito kama Fefol au Vidonge vyekundu vya kuongeza damu kwa ajili ya kuongeza damu,kuzuia watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa pamoja na Mgongo wazi,
 Dawa za Minyoo,Pamoja na Dawa za kuzuia ugonjwa wa Malaria
KUMBUKA; Baada ya kuwa Mjamzito mambo mengi hubadilika ikiwemo swala la lishe,na uvaaji- hasa kutokuvaa nguo zinazobana,au viatu virefu, na mabadiliko mbali mbali ya mwili hutokea kipindi hiki.
Kama una tatizo lolote au kuna kitu hujakielewa usisite tuwasiliane kupitia namba +255758286584 Piga au Tuma Ujumbe utajibiwa kwa haraka.

VIDONGE VYA KUONGEZA DAMU

Vidonge hivi ni maarufu kama vidonge vyekundu au FEFOL ikiwa kirefu chake ni Ferous and Folic acid. Vidonge hivi hutakiwa kutolewa kwa mwanamke akiwa mjamzito hadi wiki 6 au siku 42 baada ya kujifungua, japo wengine huacha tu baada ya kujifungua au wengine hata wakiwa na mimba wakipewa hawamezi wanatupa, Leo nikufungue macho juu ya Umuhimu mkubwa wa Vidonge hivi vya kuongeza damu.
Umuhimu wa Kuhudhuria Kliniki kwa Mjamzito,endelea kutufwatilia kujua zaidi.
UMUHIMU WA VIDONGE VYA KUONGEZA DAMU MAARUFU KAMA FEFOL AU VIDONGE VYEKUNDU
(1) Huongeza damu kwa mama,kwani Damu nyingi hupotea kipindi mjamzito anajifungua.
(2) Hupunguza Idadi kubwa ya watoto kuzaliwa na Tatizo la Mgongo wazi
(3) Hupunguza idadi kubwa ya watoto kuzaliwa na Tatizo la vichwa vikubwa
NB; VIDONGE HIVI HUSAIDIA SANA WAKATI WA UUMBAJI WA MTOTO,NA KUREKEBISHA MATATIZO MBALI MBALI AMBAYO YANAWEZA KUTOKEA KIPINDI CHA UUMBAJI WA MTOTO TUMBONI.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

147 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts ni moja ya aina...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu Tatizo la...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

 PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake) PID NI NINI?  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya kidonda mara moja. Mchakato huu...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi mkubwa baada ya watoto wawili...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali kupitia chama chao cha wafanyakazi....

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya tumbaku yana athari kubwa kwa...

148
0