LINI MAMA MJAMZITO(MAMA KIJACHO) AANZE KLINIKI?
KABLA hata mwanamke HAJABEMBA MIMBA,kama ana plan ya Kubeba MIMBA,Inashauriwa mwanamke na Mwenzi wake Wafike hospitali kwa ajili ya USHAURI na baadhi ya Uchunguzi,
lakini pia mama huyu mara moja anaanzishiwa madini kwajili ya maandalizi ya mtoto,hapa hasa ni FOLIC ACID kuzuia mtoto asije zaliwa na Magonjwa ya viungo kama Mguu kifundo,mgongo wazi,kichwa kikubwa n.k,
lakini pia kwa wenye magonjwa kama Ukimwi,presha,Homa ya ini yaani Hepatitis unaangaliwa, mfano kama Viral load Ipo chini sio risk kwa kumuambukiza mtoto na mengineyo kama ushauri wa kijumla juu ya lifestyle.
lakin sasa Kuna ile Haujajipanga,mara IMEINGIA,???
MAMA MJAMZITO ANATAKIWA AANZE CLINIC MARA TU ANAVYOGUNDUA AMEPATA UJAUZITO (umegundua una MIMBA,Plan ndani ya Wiki moja Uwe umefika Hospitali kuanza clinic na Kuonana na Dr wako)
na unatakiwa kwenda na mwenzi wako hasa kwa vipimo vya Ukimwi,hepatitis,group za damu kama Hazipo tofauti.
mfano: Unakuta mwanamke HANA MAAMBUKIZI ya VVU,mwanaume ANAYO(Discordant couple),Tukipima na kujua hili,Mnazingatia ushauri ili Kumlinda mtoto (ndio FAIDA za kuja mapema).
lakin Pia kama WOTE wanamaambukizi Pia kuna ushauri Tunatoa,Lengo ni kumlinda mtoto asizaliwe na MAAMBUKIZI.
kuna FAIDA nyingi sana za kuja kapata Uchunguzi mapema.
UMUHIMU WA MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO
➡️ Ombeni Mkumbwa
?SUMMARY
Kwa Ujumla wake safari ya kupata Mtoto huanza pale tu mwanamke anapokuwa Mjamzito mpaka atakapofikisha mda wa Kujifungua. Ambapo inaweza kuwa kutoka wiki 0-42 za Ujauzito.
VITU VYA MUHIMU KATIKA MAHUDHURIO YOTE KWA UJUMLA WAKE
➖ Kupata Elimu ya kutosha katika maswala mbali mbali ya afya kama vile; lishe,Usafi,Maandalizi ya Kujifungua,Dalili zahatari kipindi cha Ujauzito na mara tu baada ya kujifungua.
➖ Upimaji wa magonjwa kama Shinikizo la damu,Sukari,protein kwenye Mkojo,Malaria,Uti,Kasendwe,Ukimwi n.k
➖ Vipimo juu ya Group la damu la mama na wingi wake wa Damu
➖ Utoaji wa dawa za Kuzuia malaria maarufu kama SP,Dawa za minyoo maarufu kama Mebendazole,na vidonge vyekundu kwa ajili ya kuongeza damu,kuzuia watoto kuzaliwa na matatizo kama mgongo wazi na Vichwa vikubwa.
➖ Kuendelea kuchunguzwa maendelo ya mtoto tumboni ikiwemo,kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto,mlalo wake n.k
➖ Tarehe za matarijio ya kujifungua kujulikana pamoja na maandalizi kamili ya kujifungua
➖ Kuendelea kupata Elimu juu ya Njia sahihi za Kupanga Uzazi
➖ Uchomaji wa Chanjo zote muhimu kwa mama Mfano chanjo muhim ya kuzuia Ugonjwa wa PEPOPUNDA maarufu kama TETENUS
Karibu sana kusoma Makala hii na Kupata Elimu ya kutosha Juu ya Umuhimu wa Kliniki kwa Mama mjamzito
SOMO KAMILI ➡️
Mahudhurio ya Kliniki yamegawanyika katika makundi manne kulingana na Umri wa Ujauzito japo yanaweza kuzidi manne kulingana na Hali ya Ujauzito.
(1)Hudhurio la kwanza ni Ujauzito kabla ya kufika wiki 16
(2)Hudhurio la Pili ni Ujauzito ukiwa na umri wa wiki 20-24
(3)Hudhurio la Tatu ni Ujauzito ukiwa na umri wa wiki 28-32
(4)Na hudhurio la Nne ni Ujauzito ukiwa na umri wa wiki 36-40
Nb; Mahudhurio haya yanaweza kuzidi manne kulingana na Hali ya Ujauzito,mfano mama akiwa na magonjwa mengine kama presha n.k
UMUHIMU WA MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO
(1) Mama atapewa Elimu juu ya maandalizi ya kujifungua yaani INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS (IBP),Lishe wakati wa Ujauzito,Usafi wa mwili,Kujua dalili za Hatari kwa Mjamzito,n.k
?MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA
*Mama kujua vitu vya kuandaa mfano Pesa ya kutosha,Usafiri wa kwenda hosptal,Mtu atakayebaki na Familia pindi mama akiwa hospital, Kuweka vitu vyako pamoja kama kadi la Kliniki,nguo n.k, Kuwa na mtu atakayekupeleka hospital,Kuandaa vifaa kama gloves,makintosh,Chupi,pamba n.k kama vitahitajika
?BAADHI YA DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO
*kutokwa na Damu ukiwa Mjamzito
*Kutokwa na uchafu wenye harufu kali ukeni hii ni dalili ya maambukizi kama Fangasi
*Miguu kuvimba kupita kiasi,mikono pamoja na Uso
*kuona Maruerue wakati wa Ujauzito
*kutokumsikia mtoto anacheza tumboni zaidi ya masaa 24 kwa mama ambaye umri wa mtoto kucheza tumboni umefika mfano kuanzia wiki 20-24. endelea kutufwatilia kujua zaidi...
*Presha kupanda na kuwa na Protein kwenye mkojo,hiki ni kiashiria kikubwa cha Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba
(2) Mama mjamzito atapimwa magonjwa mbali mbali kama Ukimwi,UTI,Fangasi,PID,Kaswende,Malaria,Wingi wa Damu,Group lake la Damu, Presha, na Magonjwa mengine ya zinaa
(3) Mama mjamzito atasaidiwa Kujua Tarehe yake ya Matarijio kwa ajili ya kujifungua ili awe tayari.
(4) Mama mjamzito atachomwa chanjo ya kuzuia Tetenus kama hakuchoma
(5) Mama mjamzito atapewa dawa muhim sana kipindi cha Ujauzito kama Fefol au Vidonge vyekundu vya kuongeza damu kwa ajili ya kuongeza damu,kuzuia watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa pamoja na Mgongo wazi,
Dawa za Minyoo,Pamoja na Dawa za kuzuia ugonjwa wa Malaria
KUMBUKA; Baada ya kuwa Mjamzito mambo mengi hubadilika ikiwemo swala la lishe,na uvaaji- hasa kutokuvaa nguo zinazobana,au viatu virefu, na mabadiliko mbali mbali ya mwili hutokea kipindi hiki.
* Kama una tatizo lolote au kuna kitu hujakielewa usisite tuwasiliane kupitia namba +255758286584 Piga au Tuma Ujumbe utajibiwa kwa haraka.
VIDONGE VYA KUONGEZA DAMU
Vidonge hivi ni maarufu kama vidonge vyekundu au FEFOL ikiwa kirefu chake ni Ferous and Folic acid. Vidonge hivi hutakiwa kutolewa kwa mwanamke akiwa mjamzito hadi wiki 6 au siku 42 baada ya kujifungua, japo wengine huacha tu baada ya kujifungua au wengine hata wakiwa na mimba wakipewa hawamezi wanatupa, Leo nikufungue macho juu ya Umuhimu mkubwa wa Vidonge hivi vya kuongeza damu.
Umuhimu wa Kuhudhuria Kliniki kwa Mjamzito,endelea kutufwatilia kujua zaidi.
UMUHIMU WA VIDONGE VYA KUONGEZA DAMU MAARUFU KAMA FEFOL AU VIDONGE VYEKUNDU
(1) Huongeza damu kwa mama,kwani Damu nyingi hupotea kipindi mjamzito anajifungua.
(2) Hupunguza Idadi kubwa ya watoto kuzaliwa na Tatizo la Mgongo wazi
(3) Hupunguza idadi kubwa ya watoto kuzaliwa na Tatizo la vichwa vikubwa
NB; VIDONGE HIVI HUSAIDIA SANA WAKATI WA UUMBAJI WA MTOTO,NA KUREKEBISHA MATATIZO MBALI MBALI AMBAYO YANAWEZA KUTOKEA KIPINDI CHA UUMBAJI WA MTOTO TUMBONI.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!