Maana ya HIV 1 na HIV 2 Kwenye Kipimo cha UKIMWI
Virusi vya UKIMWI ni hatari sana na vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu.
Kupima UKIMWI ni njia muhimu sana ya kujua afya yako na kujiandaa kwa ajili ya matibabu iwapo utagundulika kuwa na virusi hivyo,
Kipimo cha UKIMWI kinaweza kugundua aina mbili za virusi vya HIV yaani
- HIV 1
- HIV 2.
Makala hii inaelezea maana ya HIV 1 na HIV 2 kwenye kipimo cha UKIMWI na tofauti kati ya virusi hivyo.
Tofauti Kati ya HIV 1 na HIV 2
Virusi vya Ukimwi-HIV(Human immunodeficiency Virus) vimegawanywa kwenye aina mbili, kuna HIV-1 and HIV-2.
• HIV-1 ni aina ya kwanza ya Virusi vya Ukimwi Kugunguliwa na aina hii imeenea duniani kote,
• Wakati HIV-2 ni aina ya pili na ni less pathogenic, aina hii ilithibitishwa kutokea zaidi eneo la Afrika Magharibi(West Africa) pamoja na maeneo mengine kama vile India n.k.
Kwahivo, kwa Vile tu mara nyingi hatutaji aina hizi za HIV, ila kwa asilimia kubwa tukitaja Virusi vya Ukimwi(HIV) tunamaanisha aina ya kwanza/HIV-1 maana ndyo imesambaa Zaidi Duniani kote.
Tofauti kubwa ya maambukizi ya Virusi hawa wawili(HIV-1 na HIV-2) ni kwenye mechanism ya retroviral pathogenesis, ambapo bado haifahamiki vzuri
Summary; HIV 1 na HIV 2 ni virusi viwili tofauti vya HIV. HIV 1 ni aina ya kwanza kugunduliwa ya virusi vya HIV, na inaweza kupatikana kote ulimwenguni.
HIV 2, kwa upande mwingine, ni nadra na huonekana sana katika sehemu za Afrika Magharibi.
HIV 1 na HIV 2 zina tofauti kubwa katika jeni zao, ambazo huchangia tofauti katika dalili na matibabu. HIV 1 ina jeni nyingi zaidi kuliko HIV 2, na hivyo kufanya matibabu kuwa magumu zaidi.
Maana ya HIV 1 na HIV 2 Kwenye Kipimo cha UKIMWI
Kipimo cha UKIMWI kinaweza kugundua uwepo wa virusi vya HIV 1 na HIV 2, ndyo maana utaona baadhi ya Vipimo vya Ukimwi wameandika kabsa namba 1 na 2.
Kipimo cha kawaida cha UKIMWI kinaweza kugundua protini maalum inayoitwa HIV-antigen, na kinga ya mwili inayozalishwa dhidi ya virusi vya HIV, inayoitwa HIV-antibodies.
Kipimo cha HIV(HIV 1/HIV 2) hufanyika kwa kutumia njia tofauti, ambazo ni;
- kwa kutumia kipimo cha haraka (HIV rapid test),ambapo mgonjwa huanza kupimwa, na kama kunahitajika kwenda hatua ya pili ya Vipimo basi
- Kipimo cha Uni-Gold huweza kutumika, Pia Kipimo cha UNI-GOLD ni rapid immunoassay ambapo huweza kungudua antibodies za HIV-1 na HIV-2 kwenye serum, plasma na Sampuli ya Damu kwa ujumla whole blood
- Pamoja na kipimo cha ELISA ikiwa na maana ya enzyme-linked immunosorbent assay
• Kipimo cha HIV rapid test ni rahisi na kinaweza kufanyika kwenye maabara au kliniki. Kipimo hiki kinatumia sampuli ya damu, mate, au mkojo ili kugundua uwepo wa antigeni na antibodies za HIV.
• Kipimo cha (ELISA) ni kipimo cha UKIMWI kinachotumika kutambua uwepo wa antibodies za HIV katika damu, Kipimo hiki kinaweza kugundua uwepo wa antibodies za HIV 1 na HIV 2.
Tofauti na kipimo cha HIV rapid Test, kipimo cha ELISA kinachukua muda zaidi, na kinahitaji sampuli kubwa ya damu. Hata hivyo, kipimo cha ELISA ni sahihi zaidi kuliko kipimo cha HIV rapid test.
Ikiwa mtu atapata matokeo chanya kwenye kipimo cha HIV 1 na HIV 2, inamaanisha kwamba ana virusi vya HIV mwilini. Ni muhimu kufuata ushauri wa daktari na kupata matibabu ya HIV ili kudhibiti virusi hivi na kuzuia madhara yake kwa afya ya mtu.
Kwa kawaida, mtu ambaye amepata maambukizi ya virusi vya HIV hupata matokeo chanya kwenye kipimo cha HIV rapid test baada ya wiki sita hadi nane au miezi 3 nakuendelea toka kupata maambukizi kulingana na uwezo wa Kinga yake ya mwili,
Hata hivyo, kuna kesi chache ambazo mtu anaweza kupata matokeo hasi kwenye kipimo hiki katika kipindi cha miezi mitatu hadi sita baada ya kupata maambukizi.
Ikiwa mtu atapata matokeo hasi kwenye kipimo cha HIV rapid test haimaanishi kwamba hana virusi vya HIV. Kwa hiyo, ni muhimu kufanya kipimo hiki tena baada ya wiki nne hadi sita,Pamoja na miezi 3 ili kuhakikisha.
Hitimisho
Kipimo cha UKIMWI ni muhimu sana katika kujua afya yako na kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV.
Kipimo hiki kinaweza kugundua uwepo wa virusi vya HIV 1 na HIV 2, ambavyo ni tofauti katika jeni zao na dalili zake,
Ni muhimu kufuata ushauri wa daktari na kupata matibabu iwapo mtu amepata maambukizi ya virusi vya HIV.
Kumbuka kwamba kipimo cha HIV rapid test kinapaswa kufanywa tena baada ya wiki nne hadi sita,Pamoja na miezi 3 ili kuhakikisha matokeo.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!