MADHARA YA DICLOFENAC KWA MJAMZITO

 MADHARA YA DICLOFENAC KWA MJAMZITO

Diclofenac ni aina ya dawa ambayo kwa asilimia kubwa hutumika kutuliza maumivu yaani painkiller na ipo kwenye kundi la Non-Steroidal anti-Inflammatory(NSAID's),

USHAURI,Wataalam wa afya hawashauri dawa hii kutumika wakati wa ujauzito pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa daktari,

Dawa hii haishauriwi kabsa hasa ujauzito ukiwa na wiki 30 au zaidi, badala yake mama mjamzito hushauriwa kutumia dawa kama Vile paracetum kutuliza maumivu pamoja na kushusha homa wakati wa ujauzito.

MADHARA YA DICLOFENAC KWA MJAMZITO

- Baadhi ya tafiti huonyesha kwamba Matumizi ya Diclofenac wakati wa ujauzito huongeza hatari ya mimba kutoka zenyewe yaani Miscarriage

- Matumizi ya Diclofenac wakati wa ujauzito huweza kuleta shida kwenye miezi mitatu(3) ya mwanzoni kwenye ujauzito yaani first trimester,

ambapo ndyo kipindi maalumu cha uumbaji wa viungo mbali mbali vya mtoto aliyetumboni,

Hivo diclofenac huweza kuhusishwa na kuleta madhara yaani Birth defects kwa kipindi hiki

- Matumizi ya diclofenac wakati wa ujauzito huweza kusababisha kufunga kwa mishipa kwenye moyo wa mtoto kabla ya wakati yaani premature closure of Ductus arteriosus,

Ductus arterious hutumika kupitisha nutrients pamoja na hewa safi ya oxygen kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na pia hutakiwa kufunga muda mfupi baada ya mtoto kuzaliwa sio kabla au wakati mtoto akiwa tumboni

Hivo mama mjamzito hushauriwa kuepuka matumizi ya dawa kama hizi za diclofenac hasa kwenye wiki 30 au zaidi za ujauzito

- Matumizi ya diclofenac wakati wa ujauzito huweza kusababisha tatizo la Persistent Pulmonary hypertension of newborn(PPHN),

Shida hii hutokea endapo mapafu ya mtoto kushindwa kuendana na mazingira yaliyopo

- Pia baadhi ya tafiti husema kwamba Matumizi ya diclofenac wakati wa ujauzito huweza kusababisha tatizo la maji ya uzazi kupungua zaidi yaani Oligohydramnios hasa baada ya wiki 30 za ujauzito

- Matumizi ya diclofenac wakati wa ujauzito huweza kusababisha matatizo kwenye figo za mtoto,kama vile tatizo la kidney failure,

Hii ni kutokana na baadhi ya tafiti chache ambazo zimeonyesha mtoto kuwepo kwenye mazingira ya diclofenac huweza kufeli figo zake pia.

KUMBUKA; Dawa nyingi sio rafiki kwa mama mjamzito,hivo epuka matumizi ya dawa hovio ukiwa mjamzito pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE,TUWASIALINE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!