MADHARA YA MAGADI,BAKING SODA KWA MJAMZITO
Kuna maneno mengi mtaani kuhusu matumizi ya hivi vitu Magadi au Soda ash,Baking Soda n.k kwa mama mjamzito,
Kwa leo nigusie kuhusu matumizi ya Baking Soda kwa mama mjamzito,
KUMBUKA; Shida ya kiungulia yaani heartburn huwatesa sana wanawake wengi wakiwa wajawazito kutokana na mabadiliko mbali mbali mwilini yakiwemo ya vichocheo vya mwili yaani Hormones.
Kutokana na shida hii ya Kiungulia wengi hukimbilia matumizi ya Vitu kama Baking Soda,Magadi n.k,
Matumizi ya vitu hivi sio shida sana,tatizo linakuja kwenye kiwango cha matumizi yake,
Unatakiwa utumie vitu hivi kwa kiwango kidogo sana, Unavyotumia Baking Soda wakati wa ujauzito, hakikisha kiwango kinakuwa kidogo sana na Pia inachanganyika kabsa yaani Completely dissolve.
Hii ni kutokana na kwamba Sodium iliyopo ndani ya Baking Soda, huweza kupelekea shida ya Water retention, ndyo mana hushauriwi kutumia kabsa kama tayari una shida ya kuvimba Miguu.
INGAWA,Baking Soda ni Antacid nzuri kupunguza shida ya Kiungulia,Kama ukitumia kwa kiwango kikubwa sio salama kwa afya yako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!