MADHARA YA MAZIWA YA NG'OMBE KWA MTOTO MDOGO

 MADHARA YA MAZIWA YA NG'OMBE KWA MTOTO MDOGO

Wazazi wengi pamoja na Walezi wa watoto huuliza kwamba,kwanini tusimpe tu mtoto maziwa ya ng'ombe kwa sababu ni maziwa kama maziwa mengine,

Jibu lake huweza kuwa rahisi kabsa,Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula kwa Mtoto mdogo bado haujakomaa na hauwezi kumeng'enya maziwa ya ng'ombe kwa urahisi mpaka mwisho kama ilivyo maziwa ya Mama.

Je kuna madhara yoyote endapo tutampa mtoto mdogo maziwa ya ng'ombe badala ya maziwa ya Mama yake? soma hapa chini

MADHARA YA MAZIWA YA NG'OMBE KWA MTOTO MDOGO NI PAMOJA NA;

- Maziwa ya ng'ombe yana kiwango kikubwa sana cha Proteins pamoja na Madini au Minerals kuliko kiwango kinachohitajika kwa mtoto,

Uwepo wa kiwango kikubwa sana cha proteins pamoja na madini huweza kuleta madhara kwenye Figo za mtoto ambazo hazijakomaa bado yaani Immature kidneys,

Na kusababisha madhara makubwa hasa kipindi cha joto,homa kali au wakati mtoto ana shida ya kuharisha

- Maziwa ya ng'ombe hayana kiwango cha kutosha cha madini chuma,vitamin C pamoja na virutubisho vingine ambavyo ni muhimu sana kwa mtoto wako

- Maziwa ya ng'ombe huweza kusababisha shida ya upungufu wa damu mwilini kwa mtoto kutokana na ukosefu wa madini ya chuma, hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Iron deficiency anemia

- Uwepo wa kiwango kikubwa cha proteins kwenye maziwa ya ng'ombe huweza kusababisha tatizo la miwasho au irritation kwenye kuta za tumbo pamoja na utumbo,

hali ambayo huweza kusababisha mtoto kujisaidia kinyesi chenye damu

Shida ya occult instestinal blood loss ambayo hutokea kwa asilimia 40% ya watoto wanaopewa maziwa ya ng'ombe badala ya maziwa ya mama,

- Maziwa ya ng'ombe hayana aina ya mafuta(Fat) ambayo ni salama kwa ajili ya ukuaji na afya ya mwili kwa mtoto

- Maziwa ya ng'ombe yana kiwango kikubwa sana cha Calcium pamoja na Casein,

Uwepo wa kiwango kikubwa cha Calcium pamoja na Casein huweza kuzuia ufyonzwaji wa Madini ya chuma kwenye mwili wa mtoto

- Maziwa ya ng'ombe huweza kuongeza hatari ya mtoto kupatwa na tatizo la kuishiwa na maji ya mwili yaani dehydration

- Mtoto kupatwa na shida ya allergy(mzio) au allergic reaction kwenye mwili wake kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha Proteins kwenye maziwa ya ng'ombe.

Na pia fahamu kwamba, ndani ya miezi 3 ya mwanzo,mwili wa mtoto hauna kinga ya kutosha kabsa dhidi ya magonjwa mbali mbali, hivo hutegemea kinga ya kutosha kutoka kwa maziwa ya mama yake,ambayo yana kila kitu,kila aina ya virutubisho vinavyohitajika na muhimu kwa mtoto, na pia hutoa ulinzi au kinga ya kutosha kwenye mwili wa mtoto.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!