MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO(KAMA HUKUPATA TIBA)

 MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO(KAMA HUKUPATA TIBA)

Tatizo la msongo wa mawazo huwapata watu wengi sana kwa hivi sasa kutokana na sababu mbali mbali,

Katika Dunia ya Sasa mambo yamekuwa mengi sana ambayo huweza kumfanya binadamu kupitia vipindi vigumu sana kwenye maisha yake,

Hali ambayo huchangia watu wengi kuwa na huzuni sana,wasi wasi,hofu,hasira,msongo wa mawazo,Sonona n.k

BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUSABABISHA MTU KUWA NA MSONGO WA MAWAZO NI PAMOJA NA;

- Kupoteza pesa nyingi,kukosa hela,anguko la kiuchumi

- Majanga kama vile ya mafuriko,Moto,Vitu kuungua,nyumba,biashara n.k

- Kufukuzwa kazini,

- Mtu kuibiwa vitu vyake,

- Migogoro mbali mbali kama vile migogoro ya kwenye mahusiano,ndoa,Familia au Ukoo

- Mwanafunzi kufeli mitihani yake

- Kufiwa na mtu au watu wako wa karibu sana ambao unawategemea kwa namna moja au nyingine, kama vile wazazi,ndugu na hata marafiki. N.K

DALILI ZA MTU MWENYE SHIDA YA MSONGO WA MAWAZO AMBAPO WAKATI MWINGINE HUFIKA HADI KWENYE SONONA

Mtu mwenye shida ya msongo mkali wa mawazo huweza kuonyesha dalili mbali mbali kama vile;

✓ Kuanza kujitenga sana na watu na kuanza kukaa peke yake

✓ Kukasirika haraka sana kwa vitu vidogo na vyakawaida sana

✓ Kuonekana mwenye huzuni au kukosa raha muda wote

✓ Kufanya kazi ndogo kwa muda mrefu sana, mfano mtu anaweza kufagia kaeneo kadogo tu lakini akatumia masaa anafanya kazi hyo tu

✓ Mtu kuanza kuongea mwenyewe

✓ Mtu kulia kila mara

✓ Mtu kuanza kuongea vitu ambavyo vinaashiria kujidhuru au kudhuru wengine, pamoja na kuonyesha kukosa kabsa tumaini la maisha N.K

MADHARA YA MSONGO WA MAWAZO(KAMA HUKUPATA TIBA)

Je wajua tatizo la msongo wa mawazo huweza kusababisha madhara makubwa kama halikupata Tiba?

haya hapa ni baadhi tu ya madhara ambayo huweza kusababishwa na shida ya msongo mkali wa mawazo;

• Mtu kupoteza uwezo au ufanisi wake kwenye kazi yoyote aliyokuwa anafanya

• Mtu kufukuzwa kazi kwa kushindwa kufanya kazi

• Mtu kupoteza uwezo wake wa kufanya maamuzi sahihi juu ya mambo mbali mbali anayokutana nayo

• Mtu kukosa kabsa hisia za kufanya tendo la ndoa

• Mtu kushindwa kabsa kufanya tendo la ndoa au uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume kupungua sana

• Mwanafunzi kuwa na msongo wa mawazo hadi kupelekea kufeli mitihani yake

• Maumivu makali ya kichwa

• Mtu kuanza kujiingiza kwenye vitendo vibaya kama vile; matumizi ya madawa ya kulevyia,uvutaji wa sigara,kunywa pombe kupita kiasi n.k

• Mtu kujidhuru mwenyewe au kudhuru wengine, na wakati mwingine mtu kupoteza kabsa maisha. N.K

KUMBUKA; Ukiona mtu mwenye dalili kama hizi ongea na wataalam wa afya ili mtu huyu asaidiwe haraka kabla madhara zaidi kujitokeza.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!